Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP- Boniveture Mushongi, akizungumza na waandishi wa Habari.
Miili ya watu sita wakiwa wamekufa imeokotwa katika mto Ruvu kata ya Makurunge
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akitoa Taarifa kwa waandishi wa Habari, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP- Boniventure Mushongi, Alisema
tukio hilo limebainika Tarehe 06 mwezi Desemba
2016, Saa 11 alfajiri baada ya
raia wema waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika mto huo kutoa Tarifa Polisi.
Alisema kufuatia hali hiyo Polisi walifika katika
eneo hilo na kukuta mwili wa mtu
mmoja ukiwa unaelea ambapo katika
kufuatilia imebainika miili ya watu wengine
wanne wote wakiwa wameshafariki ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-35.
Aidha, aliongeza
kuwa, siku ya Tarehe 06 Desemba
2016 ulipatikana mwili wa mtu mwingine
akiwa amekufa anakadiriwa kuwa umri
wa miaka kati ya 25- 30 na
kufanya idadi ya miili iliyookotwa
katika eneo hilo kufikia sita.
Kamanda
Mushongi alisema kuwa miili hiyo yote
ilizikwa na kwamba imekuwa vigumu kuwatambua kutokana na kuharibika
vibaya huku kukiwa hakuna kitambulisho
chochote kinachoashiria watu
hao ni
watu wa wapi
na wametoka wapi.
Alisema hali ya
miili hiyo inaonyesha
ilitupwa katika mto Ruvu na
kusafirishwa na maji kwa umbali mrefu hivyo kushindwa kubaini kwa
haraka mahali haswa mauaji hayo
yalipotekelezwa.
Jeshi
la mkoa wa Pwani
linaendelea na upelelezi ili
kubaini waliohusika kutekeleza mauaji hayo
na kwamba atakaebainika sheria itachukua mkondo wake.
Kamanda Mushon gi
amewaomba wananchi mkoani
Pwani, kutoa ushirikiano
kwa jeshi la polisi
ili kubaini watu wote wanaotekeleza uhalifu kwa namna
yoyote ile.
Katika
tukio lingine,
Kamanda Mushongi alisema
Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang'hundu wilayani Kibiti, Mohamedi Aliy
Thabiti mwenye umri wa miaka 45, amefariki
dunia baada ya kupigwa risasi na mapanga
kichwani.
Alisema tukio hilo limetokea Tarehe m05 Desemba 2016 majira ya Saa 2 :30 usiku wakati Mwenyekiti
alipokuwa anarejea nyumbani kwake akiwa
na mpenzi wake Sophia Maulidi katika
Kitongoji cha Besabu kijiji cha
Nyambunda kata ya Bungu wilaya ya
Kibiti.
Alisema
wakiwa njiani katika eneo hilo
walitokea watu watatu wakiwa
wamepakiza kwenye Pikipiki
aina Boxer isiyokuwa na namba ambapo waliwaamuru kusimama na kumpiga risasi na mapanga
kichwani.
Kamanda Mushongi
alisema mwenyekiti huyo
alifariki wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mision ya Mchukwi
kufuatia kujeruhiwa vibayasana.
Jeshi
la Polisi mkoani
pwani linaendelea na msako
wa ili kuwakamata waliohusika katika
tukio hilo.
No comments:
Post a Comment