Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu, Muyengi Bulilo, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikakijiji cha Kongo kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo.
Wananchi katika vijiji vinavyopakana na
Gereza la Kigongoni Wialayani Bagamoyo,
wameendelea kulalamikia mipaka ya Gereza hilo kwakuwa imeingia kwenye mashamba
ya raia hali inayopelekea raia kutakiwa kuondoka kwenye
maeneo wanayolima kwa muda mrefu.
Wakitoa malalamiko yao mbele ya mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo, wananchi hao wamesema hali ya kilimo imekua ngumu katika eneo linalopakana na Gereza hilo
kwakuwa tayari mkuu wa gereza ametoa amri ya kuwataka waondoke ili kupisha shughuli zinazoendeshwa na jeshi la
magereza.
Mzee mmoja akielezea kwenye mkutano huo alisema amekuwa akilima
muhogo kwa muda mrefu nakuendesha maisha
yake ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wake ambapo kwa sasa amekatazwa kulima tena katika eneo hilo hali inayosababisha ugumu wa
maisha kwakusa sehemu ya kulima.
Wananchi mbalimbali waliozungumzia mipaka ya
magereza walisema eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na mzungu aliyekuwa anajulikana kwa jina
la Mpapa toka enzi ya mkoloni
ambapo mara serikali ilipoamua kuhamishia Gereza katika shamba hilo Rais wa
awamu ya kwanza mwalimu Julias Nyerere aligawa mipaka kati ya wakulima
kutoka vijiji vinavyopakana na Gereza hilo na eneo linalopaswa kutumika na
jeshi la magereza.
Wameendelea kusema kuwa kufuatia hali hiyo
hakujawahi kutokea mgogoro wa mipaka kati ya
jeshi la magereza na wakulima mpaka ilipofika mwaka 2004 ndipo mgogoro ulipozuka baada ya jeshi la magereza
kuwataka wakulima waondoke kwenye maeneo waliyokuwa wanalima muda mrefu kwa madai ya kuwa eneo hilo ni miliki ya
jeshi la magereza.
Akijbu hoja hizo mkuu wa Gereza la Kigongoni,
Mrakibu, Muyengi Bulilo, alisema yeye ataendelea kulinda mipaka hiyo kama alivyokabidhiwa na
aliyemtangulia na kwamba hana mamlaka ya kuwaachia raia kufanya shughuli katika eneo hilo.
Alisema maeneo yote ya majeshi yanapaswa kulindwa ikiwa ni pamoja na
eneo la linalomilikiwa na Gereza
la Kigongoni na kuwataka wananchi
kuheshimu sheria ikiwa ni pamoja
na kuheshimu mipaka ya eneo la
gereza la Kigongoni.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,
Majid Hemed Mwanga, aliwataka wananchi
kuzin gatia sheria za nchi na kuheshimu maeneo yote yanayomilikiwa na
taasisi za serikali ikiwemo jeshi la magereza.
Alisema
ikiwa kuna haja ya kuwaongezea wananchi
eneo la kulima inapaswa kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kumuhusisha waziri mwenye dhamana
ili kuona namna ya kuwasaidia wananchi n
a wala sio kwa kuvunja sheria.
Wananchi wa kijiji cha Kongo wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kongo wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kongo wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga
akifuatilia maoni ya wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji
cha Kongo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga
akifuatilia maoni ya wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji
cha Kongo.
Mwananchi wa kijiji cha Kongo akichangia mada kwa ukali katika mkutano huo.
Wananchi wa kijiji cha Kongo wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara.
No comments:
Post a Comment