Mahakama ya hakimu mkazi kibaha, imemuhukumu mzee
wa baraza Francis Issaya (64) kwenda jela miaka 3 au kulipa faini laki 5 baada
ya kukutwa na hatia ya kupokea Rushwa.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Harieth Mwailolo
amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa jamuhuri
na hivyo anatoa adhabu ya kwenda jela kwa mzee huyo ili iwe fundisho kwa
wengine.
Awali mwendesha mashitaka wa Takukuru Sabina
Weston aliieleza mahakama hiyo kuwa mzee huyo wa baraza alitenda kosa hilo
mwezi uliopita kwa kumshawishi Omari Hiza ampe kiasi cha Tshs. 100,000/= ili
aweze kumsaidia mkewe Mariam Hussein aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya Jinai
329/2016 kosa Shambulio la kudhuru mwili.
Wakati huohuo Mahakama ya hakimu mkazi kibaha ya mhukumu Abduly Omar (27) mkazi wa kwa mathias kibaha kwenda jela miaka 30 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kujaribu kubaka.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya
hakimu mkazi kibaha Aziza Mbadyo alieleza kuwa mahakama imeridhika na ushahidi
uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo usio acha shaka yoyote hivyo mtuhumiwa
ataenda jela miaka hiyo ili iwe fundisho kwa wengine.
Awali mwendesha mashitaka wa serikali Lulu Ukwaju
aliileza mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 07 July 2016 huko kwa Mathias Kibaha
Abduly Omary alijaribu kumbaka binti ambaye jina linahifadhiwa kwa sasa na
kabla ya kutekeleza azima yake hiyo alikurupushwa na wanachi
No comments:
Post a Comment