Naibu Waziri wa Nishati wa kati kati Subira Mgalu akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya umeme kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya
Kisarawe pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa Tanesco, pamoja na REA, wakati
wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu.
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akiwa ameshikilia cheti maalumu
alichopatiwa na ,Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ikiwa ni ishara ya
kuonyesha jitihada zake alizozifanya katika kuchangia kampeni ya tokomeza siro
ambayo ilianzishwa kwa ajili ya wanafunzi kufanya vizuri katoka masomo
yao.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza jambo
kuhusiana na serikali ya awamu ya tano jinsi ilivyosaidia kuwaletea mradi wa
umeme kwa wananchi wake pamioja na namna utakavyoleta mabadiliko ya
kimaendeleo.
Baadhi
ya wananchi wakiwa wametulia kwa ajili ya kumsikiliza Naibu Waziri wa Nishati
Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea na
kukagua miradi mbali mbali katika sekta ya nishati ya umeme (PICHA ZOTE NA VICTOR
MASANGU).
.....................................................
VICTOR
MASANGU, KISARAWE .
WANANCHI zaidi ya elfu 38 kutoka maeneo
ya Wilaya ya Kigamboni, Ukonga, Bagamoyo, Kibaha pamoja na Wilaya
ya Kisarawe kutoka zaidi ya mitaa na vitongoji zaidi ya 62 ambao walikuwa
wanateseka kwa kipindi cha muda mrefu kukaa gizani katika makazi yao bila ya
kuwa na nishati ya umeme wanatarajia kuondokana na hali hiyo baada ya
kukamilika kwa mradi mkubwa wa kusambaza umeme Peri- Urban ambao una lengo
zaidi katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa miji.
Hayo yalibainishwa na Naibu
waziri wa nishati Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya
Kisarawe yenye lengo la kukagua na kutembelea miradi mbali mbali ya
umeme ambapo amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Namis kuhakikisha
anakamilisha mradi huo ifikapo mwezi Mei Mwaka huu lengo ikiwa ni
kuwafikishia umeme wananchi ili waweze kuutumia katika shughuli mbali mbali za
kujiletea maendeleo ikiwemo kuanzisha ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.
Mgalu alisema kwamba lengo kubwa la
serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya nishati ya
umeme sambamba na kusambaza umeme hasa katika maeneo ya vijijini kwa lengo la
kuweza kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia nishati ya umeme
kupitia miradi mbali mbali ya ujazilishi pamoja na mingine inayosimamiwa na
Tanesco pamoja na REA.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Jokate Mwegelo alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuwa ni
mkombozi mkubwa kwani kutawaondolea kero na usumbufu mkubwa wananchi hususan
kwa wale wa maeneo ya vijijini ambao walikuwa wanateseka kwa kipindi
kirefu kukaa gizani na kutoa pongezi kwa Rais wa awamu ya tano Dk. Dk
John Pombe Magufuli kwa kuweza kuboresha sekta ya nishati ya umeme katika
maeneo mbali mbali.
“Kukamilika kwa mradi huu sisi kwa
upande wetu kama Wilaya ya Kisarawe kutaweza kupunguza changamoto mbali mbali
za wananchi ambao walikuwa wanasumbuka kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa
huduma ya nishati ya umeme kwa hiyo tunapenda kumshuru sana Rais wetu wa awamu
ya tano Dr. John Pombe Magufuli kwa kuweza kutenga fedha ambazo zitaweza
kutuletea mabadiliko chanya katika sekya ya umeme, alisema Jokate.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
halmashauri ya Kisarawe akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake Hamisi
Dikupatile alibainisha kwamba licha ya kuwepo kwa changamoto ambazo zimekuwa
zikijitokeza katika suala zima la upatikanaji wa umeme lakini kwa sasa serikali
ya awamu ya tano kupitia mpango wake wa kusambaza umeme katika maeneo ya
vijijini umeweza kuwanufaisha wananchi wengi na kuwaondolea adha ya
kuishi wakiwa gizani.
Alisema kwamba serikali ya awamu ya
tano imeweza kuwaletea maendeleo wananchi wa Kisarawe kwa kuwawekea
miundombinu ya nishati ya umeme ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa
kuwainua katika kuendesha shughuli zao mbali mbali za kiuchumi na kuwaondolea
wimbi la umasikini na kuwaleta maendeleo.
“Kwa kweli sisi watu wa kisarawe
tunashukuru sana kwa Rais wa awamu ya tano Dk.Pombe Magufuli kwa kuweza
kutuleta mradi huu wa umeme ambao kwa kweli utakuwa ni mkombozi mkubwa kw
wananchi kwni walikuwa wanapata usumbufu mkubwa kutokana na ukosefu wa nishati
ya umeme hivyo kwa upande wetu ni jambo kubwa sana,”alisema Dikupatile.
No comments:
Post a Comment