Na
Omary Mngindo, Bagamoyo
MKE wa Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya
nne Mama Salma Kikwete, ambae ni Mbunge wa kuteuliwa, ameitaka jamii kushirikiana ili kukomesha
lugha za matusi zinazotolewa kwenye vituo vya mabasi.
Mama
Salma alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Zinga Kata ya
Zinga, kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake ya UWT
wilaya ya Bagamoyo, akijibu malalamiko ya Mwalimu Luciana Magige aliyelalamikia
lugha chafu vituo vya mabasi.
Alisema
kuwa vitendo vya matusi vinazidi kukithiri katika jamii, hivyo amewataka
wananchi kuwafichua kwa kuandika majina yao kisha kuyawasilisha kwa viongozi
hatimae wahusika kufikishwa vituo vya Polisi ili hatua zichukuliwe.
"Hizi
tabia za matusi zinazidi kushika kasi, kama Mwalimu Magige alivyosema kuhusiana
na matusi katika vituo vya mabasi vilivyokithiri, tuandike majina yao kisha
tuyawasilishe kwa viongozi kwenye maeneo yetu ili hatua za kisheria ziweze
kuchukuliwa," alisema Mama Salma.
Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa aliyeambatana na mbunge mwenzake
Mama Salma Kikwete, yeye alisema kuwa hali hiyo imekuwa changamoto kubwa katika
jamii, hivyo amewaomba wananchi kukomesha vitendo hivyo kwa kuweka mikakati
madhubuti.
"Kiukweli
hali si shwali katika vituo vya mabasi wakati mwingine hata mitaani, niwaombe
niwaombe wananchi wenzangu tuuchukue ushauri wa Mama Salma, kisha tuufanyiekazi
ili kukabiliana na changamoto hiyo," alisema Dkt. Kawambwa.
Awali
Mwalimu Magige aliiambia hadhara hiyo kwamba vijana wanaojihusisha na shughuli
za kuitia abiria katika mabasi wanatoa lugha za matusi hali inayiwadhalulisha
watu wazima, pia kuwaambukiza watoto lugha hizo.
Mbali
ya changamoto ya matusi katika vituo hivyo pia Mama Salma amepokea kilio cha
wasafiri wanaotokea Bagamoyo kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo wanalazimila
kupanda mabasi matatu badala ta moja kama ilivyokuwa hali awali.
No comments:
Post a Comment