NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
WAZIRI
wa mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa
Vitambulisho vya Taifa NIDA Arnold Kihaule pamoja na Menejmenti yake kufika
ofisi za Wizara hiyo siku ya jumatatu wakiwa na mpango kazi unaoonyesha
uhalisia wa kumaliza changamoto ya wananchi kupata namba za Vitambulisho kabla
ya tarehe 18, January mwaka huu.
Lugola
ametoa maagizo hayo jana katika mkutano wa hadhara na wanachi wa Mkoa wa Lindi
uliofanyika katika Viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Maagizo
hayo ya lugola yamekuja baada ya kubaini kuwepo kwa namba 17,447 za NIDA kutoka
Mkoa wa Mtwara na Ruvuma ambazo zimekamilika zikiwa bado ofisini pasipo
kuwasilishwa kwa wahusika na Vitambulisho 88,000 kati ya 117000 vilivyotengenezwa
katika Mkoa wa Lindi vikiendelea kubaki katika ofisi za NIDA.
"Pamoja
na maagizo hayo ninakutaka Mkurugenzi wa NIDA ugawe Mikoa kwa Wakurugenzi wako
na wazunguke katika hiyo Mikoa kila siku na watakapomaliza watengeneze taarifa
za kila Mkoa ambazo watakuwa wanazituma kwa katibu wa Wizara kila siku ili
tuone mwenendo wa uzalishaji na ugawaji wa namba unavyofanyika" alisema
Lugola.
Alisema
ili kukimbizana na muda uliobaki wafanyakazi wa NIDA wanatakiwa kufanya kazi
usiku na mchana ili kuhakikisha wananchi wote ambao hawajapata namba za
vitambulisho wanapata namba hizo kabla ya tarehe ya mwisho kufika bila kujali
mapumziko ya juma ama siku za siku kuu.
Maagizo
mengine aliyoyatoa Waziri huyo wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola kwa Mkuu wa
NIDA ni kuhakikisha ofisi za NIDA Zote hapa Nchini zinaongezwa wafanyakazi wa
ziada, ofisi zote za NIDA hazitakiwi kufungwa Mpaka pale mwananchi wa mwisho
aliyopo ofisini anapomalizika kupewa huduma bila kujali wingi wa watu waliopo
No comments:
Post a Comment