NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Kina
mama wajawazito wameshauriwa Kula vyakula vya aina mbali mbali vyenye Kuzingatia
lishe bora vitakavyomsaidia mtoto tumboni kuendelea kukua vizuri.
Ushauri
huo umetolewa na Muuguzi Mkunga wa kituo cha Afya cha Mji cha Manspaa ya Lindi
Mkoani humo Victoria Mrope hivi karibuni alipokuwa anazungumza na Bagamoyo
kwanza Blog.
Mrope
alisema mwili wa mama mjamzito unahitaji mlo kamili unaotokana na vyakula vya
aina mbali mbali vitakavyomsaidia kupata nguvu na virutubisho vya kutosha.
Aliongeza
kuwa miongoni mwa faida ya kula vyakula vyenye lishe kwa mama mjamzito ni
kuongeza uzito angalau kilo 12 wakati wa ujauzito kwa wastani wa kilo 1 kila
mwezi, kuboresha ukuaji wa mtoto alietumboni kimwili na kiakili, kuzuia
upungufu wa Damu.
Alizitaja
faida zingine kuwa ni Kuutayarisha mwili kwa ajili ya kunyonyesha kwa kuwa
mahitaji ya chakula na virutubisho ni mkubwa unaponyonyesha kuliko unapokuwa
mjamzito, kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye uzito pungufu pamoja na
kujifungua kabla ya wakati au kupata mtoto mfu.
Hata
hivyo Mrope pia alisisitiza kuwa mama mjamzito anapaswa kula walau milo 3 iliyokamilika
na asusa (vitafunwa ) walau mara 2 kwa siku kwa Kuzingatia makundi ya vyakula.
Nae
Mratibu wa Afya ya Uzaji katika kituo hicho cha Mji Faida Saidi alitoa tahadhari
kwa kinamama wajawazito kuepuka kula samaki au nyama mbichi au nyama isiyoiva
vizuri ili kujiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari
kwa Afya ya Mtoto alietumboni.
Tahadhari
nyingine ni Mjamzito kutoruhusiwi kula soseji au sandwich za nyama na vyakula vingine
vilivyotengenezwa kwa nyama, kwa kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya
kutengeneza vyakula kama hivyo huwa vimewekewa vihifadhi vyakula ambavyo
vinaweza Visiwe vizuri kwa mtoto alie tumboni Ulaji wa mayai mabichi au vyakula
vilivyochanganywa na mayai mabichi haruhusiwi kuliwa kwani Kuna baadhi ya 'Ice
Cream ' na Mayonaizi hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi pia
mjamzito hapaswi Kula kwa ajili ya kulinda Afya ya Mtoto alie tumboni Pia
alisema wajawazito wanashahuliwa kutokula samaki wenyekiasi kikubwa cha madini
ya zebaki.
Ulaji
wa zebaki kwa mama mjamzito umehusishwa na uzaaji wa watoto mataahira huku
akieleza mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na Dagaa wakubwa
Ulaji wa maini pia umeelezwa kuwa sio salama kwa mama mjamzito kwa kuwa kuna
kiwango kikubwa cha madini ya aina ya chuma na vitamini A ambacho vinaweza kuwa
na madhara kwa mtoto alie tumboni endapo kiwango hicho kitazidi Ulaji wa Maziwa
mabichi pia yameelezwa kuwa ni hatari kwa mtoto alietumboni kutokana na
uwezekano wa kuwepo kwa bakteria aina ya 'Listeria' ambae huweza kusababisha kuharibika
kwa mimba.
No comments:
Post a Comment