NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Halmashauri
na Wilaya za hapa Nchini zimetakiwa kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kupanga
matumizi bora ya Ardhi katika maeneo yao.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina
Mabula alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Lindi.
Wakati
wa ziara hiyo Mabula alibaini kuwa zaidi ya asilimia 66% ya vijiji vya Mkoa wa
Lindi havijapangiwa matumizi bora ya Ardhi.
Mabula
alisema ili kunusuru migogoro mbalimbali ya ardhi inayoweza kujitokeza katika
maeneo hayo ni kuhakikisha Halmashauri zinakuwa na mpango wa matumizi bora ya
Ardhi katika maeneo yote.
Aliongeza
kuwa migogoro mingi ya ardhi hasa ile ya wakulima na wafugaji hutokea pale
ambapo Halmashauri husika hazikuweka mpango shirikishi wa matumizi bora ya
ardhi katika vijiji au maeneo yao.
"Huku
tunaowakulima wengi lakini pia tunayo pia maeneo mengi ya uwekezaji sasa
tusipopanga matumizi bora ya ardhi yetu tutajikuta hatuko tayari sana kupokea
wawekezaji hivyo tunachoweza kufanya katika hili ni kuongeza kasi ya upangaji"
alisema Mabula.
Awali
katibu tawala uchumi na uzalishaji Majid muyao akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa
niaba ya Katibu tawala Mkoa wa Lindi alisema kuwa Mkoa huo una jumla ya vijiji
524 ambapo ni vijiji 176 sawa na (34%) ndivyo vyenye mpango shirikishi wa
matumizi bora ya Ardhi
No comments:
Post a Comment