Thursday, January 2, 2020

CCM YAAHIDI SIASA SAFI MWAKA 2020.

Na Silvia Mchuruza, Kagera.
 
Katibu wa chama cha mapinduzi taifa Dkt.Bashiru Ally amesema kuwa chama cha mapinduzi kinaahidi siasa safi kwa watanzania kutokana  na kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ambapo amesema hizo ni salamu za mwaka huu 2020.


Ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe pamoja na madiwani Wa Kata zote za wilaya Bukoba mkoani Kagera amewataka viongozi hao kuwa na moyo wa kufanya siasa safi ambapo amesema chama kitatetea zaidi haki za akina mama na hawatobaguliwa kutokana na nguvu yao katika jamii kuwa kubwa zaidi kwa kuwa wanawake nao wana haki kama wanaume.


Hata hivyo ameongeza kuwa hamasa kubwa ya uchaguzi imeisha kutokana na watu wenye pesa kununua uchaguzi ambapo amesema kwa mwaka huu uchaguzi utakuwa ni wa sheria na haki sawa kwa watu wote na uchaguzi unaofuata sheria za kikatiba.


” Wapo watu wanataka tume huru iwasaidie sasa niwaambie tume huru aipigi kura bali inasimamia uchaguzi na ccm ilianza kuwatafuta wapiga kura toka mwaka 1954 na ndiyo maana tunaamini tutashinda tena bila kutumia pesa au kutoa rushwa” alisema Dkt.Bashiru.


Sambamba na hayo amesema chama kimewatafuta wapiga kura kwa nguvu halali kwa kutumia siasa safi kwa kutengeneza miundombinu kama maji, umeme, Barbara, na uimalishaji wa ulinzi kwa raia wake.


“Lakini pia wapiga kura tumewatafuta kwa kuwasomesha watoto wao elimu bure,kutoka mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya huu lakini ccm aijawatafuta wapiga kura kwa kuwapa starehe kama watu wengine wanavyosema tunatakiwa kuwapa moyo ya kufanya kazi kiahalali hiyo ndiyo Ccm”


Aidha amemalizia kwa kusema chama cha mapinduzi kitaeshimu maamuzi ya umma kutokana na chama kutaka siasa safi ikiwa umma ulikiamini chama kwa mwaka ya kwanza na hats mala ya pili chama kitaaminiwa kishinde kwa kishindo.

No comments:

Post a Comment