NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo kukamilishe mapema uchunguzi dhidi
ya kasoro zilizoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019.
Pamoja
na wizi uliofanywa na viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa zao la ufuta na korosho
msimu uliopota 2018/2019 Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Amesema
pamoja na kazi nzuri waliyoifanya na inayoendelea kufanyika na Taasisi hiyo
kupitia uchunguzi na ufuatiliaji wa madai ya malipo ya wakulima wa zao la ufuta
na korosho lakini inapaswa kukamilisha uchunguzi huo mapema ili hatua za
kisheria zinachukuliwa kwa wote waliohusika Majaliwa.
Alisema
rushwa ni miongoni mwa mambo yanayoathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Kutokana
na ukweli huo, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa msukumo wa pekee katika
kushughulikia vitendo vya rushwa na ufisadi.
Msukumo
huo, umechangia kwa kiasi kikubwa hususan katika kipindi hiki, utekelezaji wa
miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ufanisi na kwa wakati.
"Kwa
mfano, upo Mradi mkubwa wa kihistoria wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere
(JNHPP) utakaozalisha Megawati 2115; Kwa uwekezaji huu pamoja na miradi
inayoendelea ya kuimarisha upatikanaji wa umeme kutumia gesi asilia na
usambazaji umeme vijijini, wastani wa upatikanaji wa Umeme vijijini umepanda
kutoka chini ya asilimia 46 mwaka 2015 hadi zaidi ya asilimia 65 mwaka
2019." Alisema Majaliwa.
Hata
hivyo, Majaliwa alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na wadau wa
mapambano dhidi ya rushwa na Utawala Bora kama vile Transparency International
(TI), MO Ibrahim na Afrobarometer zinaonesha kuwa kwa miaka mitatu mfululizo,
yaani 2016 hadi 2018 Tanzania imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi
ya rushwa na utawala bora.
Amesema
mafanikio hayo ya kujivunia ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kusimamia kwa dhati mapambano
dhidi ya rushwa kwa usimamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) ambayo ndicho chombo kilichopewa dhamana kisheria.
Akizungumzia
kuhusu jengo alilolizindua amesema muhimu sana kwa taasisi nyeti kama ya
TAKUKURU kumiliki majengo yake yenyewe.
Kuhusu
hali ya majengo ya ofisi za TAKUKURU katika ngazi ya mikoa na hata wilaya,
Awali kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana a Rushwa
(TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo amesema mradi wa jengo hilo umegharimu
kiasi cha milioni 142,857,142.86.” ambapo lilianza kujengwa 11/06/2018 na
umekamilika 25/01/2019.
Akizungumzia
kuhusu uchunguzi Mbungo alisema kwa kipindi cha mwaka 2019 TAKUKURU imefanya
uchunguzi kwenye tuhuma kubwa hasa ikiwemo wa upotevu wa fedha za wakulima wa
ufuta wa Mkoa wa Lindi Mbungo alisema Kupitia uchunguzi huo , walibaini kwamba
zaidi ya vyama 30 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vya Mkoani humo viliwadhulumu
wakulima wa zao la ufuta kiasi cha zaidi ya sh.Bilioni sh. 1.23.
Mbungo
aliongeza kuwa Kupitia uchunguzi huo waliweza kuwakamata na kuwahoji zaidi ya
viongozi 300 wa AMCOS zilizokuwa zinahusika katika dhuluma hii.
Pamoja
na kuokoa zaidi ya sh. bilioni 1.042. Ambazo zilikuwa ni mali ya wakulima wa
ufuta ambao walidhulumiwa fedha hiyo na Viongozi wa Vyama vya AMCOS.
Nae
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt Mary Mwanjelwa alitumia Fursa hiyo kuwaasa watendaji wa Taasisi hiyo
ya TAKUKURU kuyaishi yale wanayoyasema kwa wananchi kuepuka kuomba na kupokea
Rushwa ili wananchi wanaowahudumia waendelee kuwa na imani nao
No comments:
Post a Comment