Na
Omary Mngindo, Mkuranga
MAMLAKA
ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inatumia kiasi cha
shilingi bilioni 5 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji unaojengwa mwenye
hospitali ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mradi
huo unaotarajiwa kuondoa adha kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo kwa
ajili ya matibabu, hususani akina mama wanaojifungua, utakapokamilika utakuwa
mkombozi hospitalini hapo, kwani ni muda mrefu sasa wagonjwa wanakwenda na ndoo
za maji.
Hayo
yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, akitoa
taarifa ya ujenzi huo mbele ya Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo, akiwa na mwenyeji
wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiambatana na Mbunge wa
Viti Maalum Zaynab Vulu.
Luhemeja
alisema kuwa mradi huo mkubwa unaotekelezwa kwa fedha za ndani kutokana na
makusanyo ya bili za wateja wake, ni utekelezaji wa dhamira ya serikali
inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli.
"Kipekee
kabisa niishukuru serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Magufuli, jana
(juzi) tumezindua mradi mwingine mkubwa wa maji pale Kisarawe, maji yanayotokea
katika chanzo cha Mto Ruvu yanayokwenda kupunguza kama sio kumaliza changamoto
hiyo,"alisema Mhandisi Luhemeja.
Kwa
upande wake Waziri Jafo alilipongeza shirika hilo kwa ufanisi wake mkubwa
katika kusambaza maji maeneo mbalimbali, huku akisema hatua hiyo inafuatia
dhamira kubwa na njema ya Rais Magufuli ya kutatua changamoto zinazowakabili
wananchi ikiwemo ya maji.
"Sote
tu mashahidi, tangu serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu kipenzi Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli, miradi mingi ya kimaendeleo imekuwa ikitekelezwa
katika wilaya na mikoa mbalimbali, nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati ya
moyo wangu," alisema Waziri Jafo.
Kwa
upande wake Ulega nae hakusita kuishukuru serikali kwa hatua hiyo kubwa, huku
akieleza kwamba mradi huo unaojengwa hospitalini hapo, mbali ya kutoa huduma
eneo hilo, pia maji hayo yatavinufaisha vijiji mbalimbali.
"Nikuombe
ndugu yangu Jafo utufikishie salamu zetu za shukrani kwa Rais wetu John
Magufuli, hakika anatupenda sana wana-Mkuranga, leo tunashuhudia ujenzi huo
mkubwa wa tenki la maji linalolenga kuondoa changamoto husika," alisema
Ulega.
Mbunge
wa Viti Maalumu Zaynab Vulu aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa
kuyafikisha maji hospitalini hapo, huku akisema huduma ya maji pamoja na
umuhimu kwa binadamu wote, lakini wanawake ni watumiaji wakubwa wa maji.
"Tunaishukuru
serikali yetu kupitia DAWASA kwa mradi huo mkubwa Jambao leo tunaushuhudia
hapa, utakuwa mkombozi katika eneo hili la hospitali, pia kama tulivyoelezwa na
Mkurugenzi Luhemeja kwamba maji haya yatafika mpaka maeneo ya vijiji
vyetu," alisema Vulu.
No comments:
Post a Comment