Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynabu Matitu Vulu akionesha moja ya vieilelezo
vyenye taarifa mbalimbali alizochangia bungeni zinazohusu chabgamoto za
wana-Pwani, alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuia
zake kwenye Kijiji cha Kisangile Kata ya Marui Kisarawe Pwani. Picha na Omary
Mngindo.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wanawake wa (UWT) Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Sophia Gunia
akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake wa Kata ya
Marui, wakiwa katika ziara ya kuhamasisha uboreshaji wa daftari la wapigakura.
Picha na Omary Mngindo.
...................................................
Na
Omary Mngindo, Kisarawe.
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynabu Matitu Vulu, amewataka viongozi wa
kisiasa na wa Serikali kuwahimiza wananchi kujitokeza katika zoezi la
uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Zoezi
hilo linalolenga kuwapatia fursa wananchi kuhakikisha majina yao kwenye daftari
hilo, lengo kubwa ni kwa wananchi hao kuweza kusubiriki zoezi la kupigia kura
katika chaguzi zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2020, kuanzia udiwani,
ubunge na Rais.
Vulu
ametoa rai hiyo katika Kijiji cha Kisangile Kata ya Marui wilaya ya Kisarawe
mkoani hapa, akiwa kwenye ziara iliyoratibiwa na Jumuia ya Wanawake ya Chama cha
Mapinduzi (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Sophia Gunia.
Alisema
kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Feb 2
litakalodumu kwa siku saba, limeandaliwa na serikali kwa lengo la kuwapatia
nafasi wa-Tanzania kuhakiki majina yao kwenye daftari hilo.
"Serikali
imeandaa daftari hilo kwa lengo la kuwapatia fursa wananchi kuhakiki majina
yao, hatua itakayomwezesha mlengwa kupata nafasi ya kushiriki zoezi la kupiga
kura kwa kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi," alisema Vulu.
Aidha
alitolea ufafanuzi wa tofauti wa kadi ya kupigia kura na kitambulisho cha
taifa, baada ya mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Khalfan Mussa kuhoji
utofauti wa kadi hiyo ya kupigiakura na kitambulisho cha taifa.
Kwa
upande wake Sophia ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo alisema kwamba, zoezi
hilo litakalodumu kwa wiki moja halitakuwa na muda wa nyongeza, hivyo amewaasa
wana-Kisarawe kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kuwa na haki ya kuchagua na
kuchaguliwa.
"Tusijiingize
katika kadhia ambayo hivi sasa wananchi wengi imetukuta inayohusiana na
kitambulisho cha Taifa, tulitangaziwa kipindi kirefu kuhusiana na zoezi hilo,
lakini tulipuuza hatimae hivi sasa tunahangaika na kuitupia lawama
Serikali," alisema Mwenyekiti huyo.
Diwani
wa Kata hiyo Salehe Mfaume alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo likifika
linafanyika kwa mafanikio makubwa, huku akiwaasa viongozi wa ngazi zote
kushirikiana kwa lengo la kulifanikisha.
No comments:
Post a Comment