|
|
NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
WAZIRI
MKUU Kasimu Mjaliwa amempongeza jaji mkuu wa Tanzania Profesor Ibrahim Juma kwa
kutumia teknolojia ya ujenzi wa gharama nafuu (MOLADI) inayoiwezesha Mahakama
kujenga mahakama nyingi zenye ubora ,kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.
Majaliwa
aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa
Mkoani Lindi, Lenye thamani ya Shilingi milioni 780.
Majaliwa
Alisema mahakama ndio chombo cha kwanza kilichoweza kumuunga mkono Rais wa
jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK, John Pombe Magufuli, kwa kutumia vizuri
fedha ya Serikali
“kama
ambavyo mmesikia jengo hili na thamani yaeke ni milioni 780, nataka niwajulishe
gharama hii ni ya chini ukilinganisha na zabuni zilizokuwa zinatolewa za
kujenga mahakama, na hiyo ndio ilikuwa inafanya mahakama nyingi Nchini
zikashindwa kujengwakwa sababu ya gharama.
“hata
mahakama hii pamoja na mahakama hile ya kibaa na mahakama zilizotangulia, baada
ya kuwa zimerushwa zabuni kutafuta wazabuni wa kujenga zilipatikana zabuni
mbili ambapo mzabuni wa kwanza alitaka kujenga kwa bilioni moja na milioni mia
saba na mzabuni wa pili alitaka kujenga kwa bilioni moja na milioni miatano ,
mahakama iliacha na wakasema watatafuta utaratibu wa kujenga ambao ni wakutumia
(MALODI)” aliongeza Majaliwa.
Majaliwa
alisema mahakama ni chombo muhimu katika kudumisha amani na kuleta maelewano
ndani ya Nchi au jamii kupitia mahakama migogoro mingi hupata usuluishi na
hivyo kuimarisha hali ya amani na utulivu.
Aliongeza
kuwa Mahakama inapokuwa imara Taifa letu hubaki salama na kufanya wananchi
waliopo katika taifa hilo kuendelea kufanya kazi zao za kujiletea maendeleo
hivyo mahakama ni mhimili muhimu katika Nchi.
Awali
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesor Ibrahim Juma alisema kuwa kwa muda mrefu,
Mahakama ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba, na
uchakavu wa majengo katika ngazi zote za Mahakama, yaani—Mahakama za Mwanzo,
Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi (Mahakamaza Mikoa), Mahakama Kuu
na hata Mahakama ya Rufani.
Alisema
Ili kukabiliana na ukubwa wa changamoto ya upungufuna na uchakavu wa majengo
yake, Mahakama ya Tanzania ilitayarisha Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya
Miundombinu (2016-2021). Ambao umetathmini hali ya majengo ya Mahakama katika
Mikoa na Wilaya zote za Tanzania Bara, ambao umelenga kupunguza au kuondoa
kabisa uhaba na uchakavu. Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa ni
kielelezo cha utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Miundombinu
ya Mahakama ya Tanzania.
Hata
hivyo aliongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa miradi iliyokamilika,inayoendelea na
ile iliyopo hatua za kukamilika, hivi karibuni wanatarajia kuanza miradi mipya
katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Lindi.
Miradi
hii yote inayotekelezwa ni matokeo ya mikakati na mipango madhubuti
waliyojiwekea kama taasisi kupitia mpango mkakati wa miaka mitano Nae Bashiru
kauchumbe Mkazi wa Wilaya ya Ruangwa aliishukuru serikali ya Awamu ya Tano kwa
kuwasogezea karibu huduma hiyo ya kimahakama kwani hapo awali walilazimika
kusafiri umbali wa kilomita 180 kufuata huduma hizo za mahakama ya wilaya mjini
Lindi.
“Wapo
wananchi wengi, ambao kwa umbali huo hadi mjini Lindi, waliamua kuacha kufugua
mashauri yaliyostahili kufunguliwa mahakama ya wilaya kwa hatua zaawali.
Wapo
pia wale ambao walishindwa kutafuta haki ya rufaa katika Mahakama ya Wilaya.
Hata kwa wale walidhubutu kwenda Lindi, umbali huo uliwaathiri kwa kutumia muda
wao mwingi kutafuta huduma za Mahakama, badala ya kuendelea na shughuli zao za
kiuchumi na kijamii” alieleza mwananchi huyo.
No comments:
Post a Comment