Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta katikati mwenyesuti, akiwa na Kaimu
Mkurugenzi Mahudu Kazi wa kwanza kulia, Luteni Kanali wa JWTZ David
Luoga wakipitia nyaraka za mkataba wa ujenzi wa Jengo la Utawala pamoja na
Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu.
Luteni Kanali wa JWTZ David Luoga,
akiwaonyesha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamini
Sitta, Kaimu Mkurugenzi Mahudu Kazi, mchoro wa uwanja wa mpira wa miguu
utakavyokuwa. Mwenye shati la kijani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Kinondoni Mhe. Harlod Muruma.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta mwenyesuti akipeana mkono na Luteni
Kanali David Luoga wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya
kusaini mkataba na ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Jengo la Utawala
pamoja na Uwanja wa mpira wa miguu.
...................................
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi Tanzani (JWTZ) kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja
wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Jengo la kisasa la Utawala la Halmashauri
hiyo.
Mkataba huo umesainiwa jana Januari 27,
2020 na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Benjamini Sitta pamoja na Luteni
Kanali David Michael Luoga na kushuhudiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo
pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni
Harlod Maruma.
Akizungumza na wandishi wa habari
wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Mhe. Meya Sitta amesema kuwa mradi wa
ujenzi wa jengo la utawala utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 huku
ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigharimu kiasi cha shilingi
Bilioni 2.7.
Amefafanua kuwa uamuzi wa kutumia JWTZ
umetokana na kufuata ushauri uliokuwa unatolewa na Mhe. Rais Dk. John Pombe
Magufuli wakutumia Locol Fundi (Foce Account).
Mhe. Meya amesema kuwa miradi hiyo
mikubwa miwili iliyosainiwa itajengwa na
Jeshi la Wananchi kwakuwa wana amini watafanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa na
wa haraka kulingana na mkataba huo ulivyoeleza.
“ Tunamshukuru Mhe. Rais wetu
mpendwa, Dk. Magufuli kwa kutuonyesha njia ya kufanya kazi kwa kutumia
wanajeshi kwa kuwa itakamilika kwa wakati, hapa hakuna michakato, miradi hii
mikubwa itafanywa na jeshi la JWTZ” amesema Meya Sitta.
Aidha Mhe. Meya Sitta alisema
wanampongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuwa msikivu na kufuata maelekezo.
“tunampongeza Mkurugenzi wetu Aron
Kagurumjuli, kwakweli tuna mkurugenzi makini, msikivu ,ambaye anafuata
maelekezo na ni mchapakazi ndio mana leo Kinondoni yetu ipo hapa” alisema.
Kwa upande wake Luteni Kanali Luoga
ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na kuahidi
kukalimisha ujenzi huo kwa muda wa miezi sita.
Luteni Luoga amesema katika ujenzi wa
uwanja wa mpira wa miguu, awamu ya kwanza itakamilika kwa kipindi cha miezi
mitatu na nusu na awamu ya pili itatumia miezi miwili na nusu.
Ameongeza kuwa katika ujenzi huo, licha
ya kwamba Jeshi la Wananchi litafanyakazi hiyo, lakini pia litatoa nafasi kwa
watu wengine ikiwemo Mama ntilie pamoja na vijana wengine lengo likiwa ni kila
mwananchi apate kipato.
“ Tunampongeza Mhe. Meya Sitta,
Mkurugenzi Kagurumjuli kwa kutuamini, nasisi tunawahakikishia kuwa Jengo la
utawala pamoja na uwanja tutakamilisha kwa kipindi cha miezi sita kama ilivyo
kwenye mkataba wetu”amesema Luteni Kanali Luoga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma amefafanua kuwa ujenzi huo wa miradi
mikubwa miwili iliyotiwa saini leo ni utekelezaji wa ilani CCM.
Imetolewa na Kitengo Cha Habari na
Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment