Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kisarawe akizungumza na wananchi wa kata ya Msanga hawapo pichani wakati
wa ziara yake ya kikazi kwaajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo
katika Wilaya ya Kisarawe.
..................................................
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
KINAMAMA wa kata ya Msanga Wilayani
Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na kilio cha muda mrefu cha
kutembea umbari mrefu wa zaidi ya kilometa 15 kwa ajili ya kwenda
kupatiwa matibabu katika maeneo mengine hatimaye wamepata mkombozi baada ya
serikali ya awamu ya tano kutoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya
ujenzi wa Kituo cha afya ambacho kitasaidia kupunguza vifo vinavyotokea
wakati wa kijifungua.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Miko na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo
wakati wa ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe yenye
lengo la kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya
na elimu sambamba na kuzungumza na kusikiliza kero na changamoto za
wananchi ambapo ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa halmashauri ya
Kisarawe kukamilisha ujenzi huo wa kituo cha afya.
Aidha Jafo alisema kwamba lengo kubwa
la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya
katika maeneo mbali mbali ikiwemo kuimarisha miundombinu ya majengo pamoja na
kuongeza vifaa tiba katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali
lengo ikiwa ni kutoa huduma nzuri ya matibabu kwa wananchi wote.
“Katika sekta ya afya katika kipindi
hiki cha miaka minne kwa kweli tumeweza kupiga hatua kubwa sana kwani baaadhi
ya maeneo katika Wilayah hii ya Kisarawe kulikuwa hakuna kabisa zahanati wala
vituo vya afya lakini kwa sasa mambo yamebadilika kwani kumejengwa vituo vya
afya vipya katika baadhi ya kata pamoja na zahanati hii yote ni kuhakikisha
kwamba wananchi wetu hawapati usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa matibabu na
ndio maana serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kituo cha
afya cha Msanga.”alisema Jafo.
Kwa upande wao baadhi ya kinamama wa
kata ya Msanga wamesema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya kutaweza
kuwapunguzia kero na changamoto mbali mbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo
hasa pindi wanapokwenda kujifungua kwani wanatumia usafiri wa baiskeli na
bodaboda kwenda kupatiwa matibabu kwingine kitu ambacho ni hatari kwa usalama
wa maisha yao na kutoa pongeza za dhati wa serikali ya awamu ya tano
katika kuboresha sekta ya afya.
Walisema kwamba katika kata ya Msanga
kumekuwepo na changamoto kubwa katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya
afya hasa kwa kinaamama japo kuwa na zahanati hivyo wana imani pindi ujenzi huo
utakapokamilika utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa ile changamoto ya
kujifunguliwa njiani.
“Kituo hiki cha afya pindi
kitakapokamilika kwa upande wetu sisi kama wananchi wa kata hii ya msanga
hususan kwa upande wa wakinamama tumekuwa tukipata usumbufu mkubwa sana wa
kwenda umbari mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya matibabu katika maeneo
mengine ikiwemo kituo cha afya Manelumango hivyo baada ya miezi mitatu hali hii
kwetu itakuwa ni historia kwa hiyo tunamshukuru sana Mbunge wetu Jafo pamoja na
Rais we Dk John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi milioni 400 za ujenzi
,”walisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Musa Gama ameahidi kulitekeleza na
kulisimamia agizo hilo la mradi wa ujenzi wa kituo cha afya lengo ikiwa ni
kuwaondolea wananchi changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda
kupatiwa matibabu katika maeneo mengine na kumpongeza Rais wa awamu ya tabo
Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo.
“Kwa
kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Rais wetu Dk. John Pombe
Magufuli pamoja na Mbunge wetu Seleman Jafo ambaye ni Waziri wa Tamisemi kwa
kuona umuhimu wa kutupatia fedha hizi kiasi cha shilingi miliono 400 kwa ajili
ya ujenzi wa kituo cha afya na mimi naahidi kusimamia ujenzi huu kwa hali na
mali lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma ya matibabu
karibu.”alisema Gama.
KUKAMILIKA kwa mradi wa ujenzi wa
kituo kipya cha afya ambacho kinajengwa katika kata ya Msanga
Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa
wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbari mrefu pamoja na kuondokana
na usumbufu mkubwa waliokuwa wakiupata kinamama wajawazito kwa kipindi kirefu
pindi wanapotaka kwenda kujifungua.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Msanga
wilayani Kisarawe wakimsikiliza kwa umakini Waziri Jafo ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kisarawe hayupo pichani wakati akiwahutubia wananchi hao katika
mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero
pamoja na changamoto za wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Kisarawe kushoto Mussa Gama akiwa katika mkutano wa adhara ambao
umeitishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
(TAMISEMI) Selemani Jafo, kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha
mapinduzi CCM wakisikiliza maagizo ya Waziri Jafo mara baada ya kutembelea
ujenzi wa zahanati ya Kwala ambayo inajengwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya
afya kwa wananchi.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za
mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kisarawe kulia akitoa maelezo kwa viongozi wa Chama cha amapinduzi CCM
na baadhi ya viongozi wa halmashauri alipotembnelea mradi wa ujenzi wa kituo
cha afya chole.
Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama akiwa anapokea maagizo ambayo
yalikuwa yanatolewa na Waziri Jafo hayupo pichani wakati wa ziara hiyo ya
kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za
mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kisarawe akisalimia na baadhi ya viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM
kata ya Msanga baada ya kuwasili katika eneo hilo akiwa katika ziara yake ya
kikazi kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na kukagua miradi ya
maendeleo. (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment