WANANCHI 10,378 WAFIKIWA NA HUDUMA YA AFYA YA MACHO LINDI.
NA HADIJA OMARY, LINDI. Jumla ya Wananchi 10,378 kutoka halmashauri sita za Mkoa wa Lindi wamefikiwa na huduma ya Afya ya macho ambapo kati yao 9690 wamefanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu Hayo yameelezwa na Dokta Sharifu Hamza kwa niaba ya Mganga Mfawidi wa hospital ya Rufaa MKoa wa Lindi Sokoine, Jana oktoba 10 wakati wa maadhimisho ya Afya ya macho yaliyofanyika kimkoa Katika hospital hiyo ya Rufaa Sokoine huko Manispaa ya Lindi . Zoezi hilo la utoaji Elimu ya Afya ya macho sambamba na vipimo na matibabu limeendeshwa kwa ufadhili wa mashirika ya Heart to Heart foundation, CBM pamoja na Korea church . Amesema zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku saba kuanzia oktoba 4 hadi 10 wataalamu walipita katika shule mbalimbali kwa halmashauri zote sita kutoa elimu pamoja na kutoa matibabu kwa wananchi walioonekana na changamoto ya afya ya macho. maadhimisho hayo ya Afya ya macho yanayohimiza vijana na watoto kupenda macho yao na kuitaka dunia kuonge...