Popular posts from this blog
RAIS SAMIA AKIPEWA POLE NA VIONGOZI MBALIMBALI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamona na Viongozi mbali mbali wa Vyama na Serikali na Wananchi, wakimfariji Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipofika nyumbani kwake Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, kufuatia kufiwa na Mume wake Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Mzena Zanzibar, tarehe 07 Sept, 2026.
SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO. Na Athumani Shomari Bagamoyo. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga amechangia mifuko 50 ya Cement kwaajili ya ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Msingi Sirajulmunir iliyopo kata ya Nianjema wilayni Bagamoyo. Mkuu huyo wa wilaya ametoa Ahadi hiyo hivi karibuni, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya wahitimu wa darasa la saba, katika shule hiyo. Akizungumza kwa niaba yake, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya, Ibrahim Gama amesema juhudi zinazo oneshwa na shule hiyo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ndani na nje ya Bagamoyo. Amesema Watoto wanaosoma Shule ya Sirajulmunir wana uwezo mkubwa katika masomo hali inayopelekea kila mwaka kufanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na wanakuwa Watoto wenye maadili mema katika jamii. Aliongeza kwa kusema kuwa, ufasaha wa lugha ya kingereza, kiarabu, ufaulu mzuri na maadili mema ni Ishara kubwa ya ubora wa elimu inayotolewa s...
THE ISLAMIC FOUNDATION YAMKABIDHI CHEREHANI ALIYEMALIZA KIFUNGO GEREZANI.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
Taasisi ya The Islamic Foundation yenye Makao yake Makuu Mkoa wa Morogoro imetoa msaada wa cherehani kwa Issa Mohamed Kitambi, aliyemaliza kifungo cha miaka minane katika Gereza la Mahabusu Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono katika kuanza maisha mapya baada ya kutoka gerezani. Issa ambaye alipata mafunzo ya ushonaji akiwa gerezani, sasa anatarajiwa kutumia cherehani hiyo kuendeleza ujuzi alioupata na kujiajiri kupitia kazi ya ushonaji wa nguo. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa The Islamic Foundation, Arafat Badru, amesema wameguswa na jitihada zinazofanywa na Jeshi la Magereza za kuwapatia wafungwa mafunzo ya ujuzi, ili wanapomaliza vifungo vyao wawe na uwezo wa kujitegemea. Amesema cherehani hiyo imelenga kumpa Issa nyenzo ya kuanzia katika kazi yake na kumsaidia kuendesha maisha yake baada ya kumaliza kifungo. Akizungumza katika zoezi hilo, Mkuu wa Gereza la Mahabusu Morogoro, Mrakibu wa Jeshi la Magereza (SP) SabaS...
KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU Na Albert Kawogo Jumatano 9 Septemba 2026 RAIS wa awamu ya nne , Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika sekta za uzalishaji na usalama wa chakula, teknolojia, uvuvi na uchumi wa buluu. Dkt. Kikwete ameyasema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Sasakawa Peace Foundation ya Japan, Bw. Masanori Kobayashi, katika ofisi yake ndogo iliyopo Masaki, Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalilenga kufuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa wakati wa ziara ya kikazi ambayo Dkt. Kikwete alifanya nchini Japan kuanzia Julai 23 hadi 24, 2025. Katika ziara hiyo, Dkt. Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi sita mashuhuri kutoka Afrika walioalikwa na Serikali ya Japan kupitia taasisi za Sasakawa Peace Foundation na Nippon Foundation. Viongozi hao walishiriki katika kutoa ushauri kuhusu namna bora ya...
MUME WA RAIS DKT. SAMIA AFARIKI DUNIA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MUME WA RAIS DKT. SAMIA AFARIKI DUNIA. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametangaza kifo cha Mhe. Hafidh Ameir Hassan ambaye ni mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kilichotokea leo Septemba 07, 2026 majira ya saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo. Mipango ya mazishi inaendelea kufanyika Kizimkazi Zanzibar
RC PWANI KUENDELEZA AGENDA YA UWEKEZAJI NA KUWAJENGA VIJANA KIUCHUMI
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
RC PWANI KUENDELEZA AGENDA YA UWEKEZAJI NA KUWAJENGA VIJANA KIUCHUMI Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, amesema ataendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kukuza uwekezaji na uchumi wa Mkoa wa Pwani, huku akisisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kiuchumi. Mhe. Nyongo amesema hayo leo, Septemba 8, 2026, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Abubakar Mussa Kunenge, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Amesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa maeneo muhimu kwa uwekezaji nchini na kwamba atashirikiana na viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa rafiki kwa wawekezaji. “Mkoa huu ni wa uwekezaji. Nimezunguka maeneo mbalimbali kutafuta wawekezaji, kwa hiyo niwakaribishe kwa kuweka mazingira wezeshi,” amesema Mhe. Nyongo. Aidha, Mhe. Nyongo ameomba ushirikiano wa jamii katika kuwajenga na kuwawezesha vijana kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yanayo...
KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA. Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi (CP) Tatu Jumbe, Septemba 09, 2026 amepokea ugeni kutoka Magereza nchini Malawi ukiongozwa na Kamishna Milda Salilika ambaye ni Kamishna wa Urekebu na utengamanisho huduma za Magereza Malawi, uliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania mkoani Dodoma kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF Net) unavyofanya kazi. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, CP Tatu Jumbe ameeleza umuhimu wa kubadilishana uzoefu baina ya taasisi za ulinzi na usalama za Tanzania na Malawi, akibainisha kuwa ushirikiano wa aina hiyo unatoa fursa ya kujifunza mifumo bora na kubaini maeneo ambayo yanaweza kuboreshwa kwa manufaa ya askari na taasisi kwa ujumla. Kwa upande wake, Kamishna Milda Salilika kutoka Magereza nchini Malawi, ameeleza namna a...
MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza Mamlaka na Taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kujiandaa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026. Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea taarifa ya utayari na maandalizi ya Serikali kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mvua za El- nino, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Viongozi pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zilizochini ya Wizara hizo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa taasisi zote zinazohusika, kufanya kazi kwa pamoja na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kuzuia au ku...
















Comments
Post a Comment