BEI ZA MAFUTA SEPTEMBA ZASHUKA NCHINI

 

BEI ZA MAFUTA SEPTEMBA ZASHUKA NCHINI


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2026. 



Bei ya petroli imeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa Shilingi 101 kwa lita. Bei hizo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 2 Septemba 2026, saa 6:01 usiku.


EWURA inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, ambapo mabadiliko ya bei yanaendelea kuathiriwa pamoja na mambo mengine na hali ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.


Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015, bei za mafuta zinaendelea kupangwa kwa kuzingatia mfumo wa soko.



Wafanyabiashara wote wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zisizozidi bei elekezi, na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa EWURA kwa kituo chochote cha mafuta kitakachouza zaidi ya bei elekezi.


Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

UONGOZI WA AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YAJIDHATITI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA KUISAIDIA JAMII

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016 HAYA HAPA.

MELI YA MV CHAMBO YATEKETEA KWA MOTO.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU KWA WASANII TOZO ZIKIPUNGUZWA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.