KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA.
KAMISHNA WA MAGEREZA MALAWI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA.
Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna wa Polisi (CP) Tatu Jumbe, Septemba 09, 2026 amepokea ugeni kutoka Magereza nchini Malawi ukiongozwa na Kamishna Milda Salilika ambaye ni Kamishna wa Urekebu na utengamanisho huduma za Magereza Malawi, uliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania mkoani Dodoma kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF Net) unavyofanya kazi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, CP Tatu Jumbe ameeleza umuhimu wa kubadilishana uzoefu baina ya taasisi za ulinzi na usalama za Tanzania na Malawi, akibainisha kuwa ushirikiano wa aina hiyo unatoa fursa ya kujifunza mifumo bora na kubaini maeneo ambayo yanaweza kuboreshwa kwa manufaa ya askari na taasisi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Kamishna Milda Salilika kutoka Magereza nchini Malawi, ameeleza namna ambavyo wamejifunza kuhusu uendeshaji wa Mtandao wa Askari Wanawake , hususan katika kuwawezesha askari wanawake kushiriki kikamilifu katika majukumu ya kiuongozi na kitaaluma.
Aidha, wameweza kuufahamu kwa kina muundo na utendaji wa TPF Net, ikiwemo namna mtandao huo unavyowaunganisha askari wanawake, kuwajengea uwezo na kushirikiana katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo, ustawi na nafasi ya wanawake ndani ya Jeshi la Polisi na pia namna ya kutoa huduma kwa wananchi.






Comments
Post a Comment