MKUU WA MKOA ARUSHA AKUTANA NA WENYE HOTELI NA WADAU WA UTALII

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Septemba 24, 2026 amekutana na kuzungumza na Wamiliki wa Kampuni za Utalii, wamiliki wa Hoteli, Waongoza watalii, wamiliki wa kumbi za burudani, wapagazi na wasanii wa Mkoa wa Arusha, akiwataka kutumia vyema fursa za ujio wa Bunge la dunia (IPU) linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 05, 2026 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).


"Wabunge wa IPU watakuwa zaidi ya 2, 500 na kila Mbunge ana msaidizi wake na wengine watakuja na familia na wapo wanaopanga kwenda kutalii, sasa hii ni fursa na nimeona niwaambie ili mchangamkie fursa hii, watu hao watalala kwenye hoteli zetu, watakula kwenye migahawa yetu, watataka kwenda kuona vivutio na zaidi watu hawa wakija wanaangalia pia vitu vingine kama uwekezaji, biashara na kupanga kurudi tena- Wakichagua huduma yako hakikisha unawaachia tabasamu warudi tena kwako na niwaombe Tanzania inajulikana kwa amani na ukarimu na sisi tukatoe taswira hiyo wakati wa kutoa huduma zetu." Amesema Mhe. Makalla.


Kwa upande wao washiriki wa Kikao hicho cha Mkuu wa Mkoa, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuifanya Arusha kuwa kitovu cha utalii wa hifadhini na Utalii wa Mikutano, wakiahidi kutekeleza maelekezo yote ya Mhe. Makalla wakati wote wa Bunge hilo la dunia pamoja na kujiandaa kikamilifu kuelekea michuano ya AFCON mwaka 2027 ili kuitangaza sifa njema ya Tanzania Kimataifa. 





Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

GURUMO AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA NA WAZIRI KIKWETE

TAKUKURU KAGERA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 2.

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

GREEN ACRES YAANZA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA