SUBIRA MGALU AULIZA HATUA YA FIDIA KWA WANANCHI WA BARABARA YA MAKOFIA–MLANDIZI
SUBIRA MGALU AULIZA HATUA YA FIDIA KWA WANANCHI WA BARABARA YA MAKOFIA–MLANDIZI
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamis Mgalu, ameuliza Serikali kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kuwalipa fidia wananchi wanaopitiwa na mradi wa Barabara ya Makofia–Mlandizi katika Kata ya Yombo.
Akitoa swali la nyongeza, Mhe. Subira amesema barabara hiyo imefungamanishwa na mpango wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na eneo la viwanda la Kwara, hivyo umuhimu wake unaendelea kuongezeka.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema kuwa Wizara tayari imekamilisha tathmini ya fidia na imewasilisha mahitaji hayo katika Wizara ya Fedha.
Amesema Serikali inaendelea na taratibu za kupata fedha, na mara fedha zitakapopatikana, wananchi waliostahili watalipwa fidia ili hatua za ujenzi wa barabara hiyo ziweze kuendelea.

Comments
Post a Comment