TARURA YATENGA BIL. 1 KUKABILIANA NA EL NINO TABORA

 

TARURA YATENGA BIL. 1 KUKABILIANA NA EL NINO TABORA 


Na Allan Kitwe, Tabora


WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoani Tabora wametenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ili kukabiliana na wingi wa mvua za el nino.


Hayo yamebainishwa jana na Afisa wa Wakala huo, Mhandisi Nehemia Chacha kwa niaba ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Tabora alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya barabara kwenye kikao cha madiwani wa halmashauri ya manispaa.


Ameeleza kuwa ili kuhakikisha miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo inapitika wakati wote wamekamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 2 ya kimkakati katika kata za Ndevelwa, Misha na Kabila.


Mhandisi amefafanua kuwa daraja la Ndevelwa ambalo lilikuwa kero kubwa sana kwa wananchi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 460 na limekamilika kwa asilimia 100 na sasawananchi wameanza kulitumia, kero imeisha


Daraja la pili ni lile linalounganisha Kata za Misha na Kabila ambalo lilikuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa wakazi wa Vijiji vya Igambiro na Igombe, nalo limekamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya shilingi milioni 592.


‘Miradi hii imekamilika kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha maeneo korofi yote yanashughulikiwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa kero hiyo’, amedokeza.


Aidha kuelekea msimu ujao wa mvua, alisema kuwa TARURA imetenga kiasi cha shilingi milioni 950 kwa ajili ya matengenezo ya mifereji kwenye kingo za Mto Kenge ili kuepusha mafuriko ambayo yamekuwa yakiathiri shughuli za wananchi.


Mto huu umekuwa ukisababisha adha kubwa na kuathiri shughuli za wananchi katika kata za Kanyenye, Kitete, Mwinyi na Malolo na kusababisha mafuriko kila mwaka punde mvua zinapoanza kunyesha, tatizo hili sasa litabaki historia.


Mradi mwingine ni ule utakaotekelezwa na vikundi 8 vya vijana ambao umetengewa kiasi cha shilingi milioni 121 ambapo kazi zitakazofanyika ni matengenezo ya kawaida katika barabara korofi zote na kufukua mifereji yote.



Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

UONGOZI WA AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YAJIDHATITI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA KUISAIDIA JAMII

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016 HAYA HAPA.

MELI YA MV CHAMBO YATEKETEA KWA MOTO.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU KWA WASANII TOZO ZIKIPUNGUZWA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.