MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI, MHESHIMIWA NETO PAUL KAPALATA AFANYA ZIARA NA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KATA YA UGEMBE.

 

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI, MHESHIMIWA NETO PAUL KAPALATA AFANYA ZIARA NA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KATA YA UGEMBE.

Nzega Vijijini, Nzega, Tabora.

Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Mheshimiwa Neto Paul Kapalata, ameendelea na ziara zake za kata kwa kata kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Katika ziara na mkutano wa hadhara wa kata uliofanyika katika kijiji cha Ugembe, mheshimiwa Kapalata aliambatana na Afisa wa tarafa ya Puge, wataalamu kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wakala wa Maji na Usafi Wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme ya Tanzania (TANESCO) na wataalamu wa ngazi ya kata, vijiji na vitongoji husika ili kupokea kero, changamoto na maoni ya wananchi na kutoa ufafanuzi kuhusu hatua sahihi zitakazochukuliwa katika utatuzi.

Akizungumza katika ziara na mkutano wa hadhara, Mheshimiwa Kapalata pamoja na wataalamu walijibu kero, changamoto na maoni kwa kudadavua kwa kina kila kilichojili na mwisho aliwashukuru wananchi wa Jimbo la Nzega Vijijini kwa kumpa imani na kumchagua Daktari Samia Suluhu Hassan kuwa mwakilishi wao wa nafasi ya urais, yeye binafsi nafasi ya ubunge na madiwani nafasi za udiwani, huku akisisitiza kudumisha hekima, umoja na amani na kuahidi kuendelea na utaratibu wa kuwa karibu na wananchi ili kusikiliza, kushughulikia na kutatua kero na changamoto kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi katika sekta zote husika. 

Aidha, ziara hii ni sehemu ya utekelezaji ilani ya 2025 - 2030 ya Chama Cha Mapinduzi na ahadi binafsi kama Mbunge na kuendelea kushirikiana na wananchi na serikali ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma stahiki na maendeleo endelevu yanawafikia wananchi kwa wakati kwa mstakabali sahihi

Na Antony Paschal Lugai
Afisa Habari
Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini, Nzega, Tabora







Comments

Popular posts from this blog

RAIS DKT. SAMIA AKIWA PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS DEOGRATIUS NDEJEMBI.

WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA

MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA

MAKAMU WA RAIS AWASALIMU WANANCHI WA CHAMWINO

GLOBAL YASAFIRISHA KUNDI LINGINE LA WANAFUNZI KWENDA NJE YA NCHI.

OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA, YAMPONGEZA NDEJEMBI.