MWENYEKITI MBEYA DC ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA SHULE

 

MWENYEKITI MBEYA DC ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA SHULE


Wananchi wa Kitongoji cha Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, wamejiunga pamoja na kuanza kuchimba msingi kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Eneo la Shigamba Pipeline ambalo wananchi hao wamejitolea, ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 583, hatua inayotajwa itasaidia kuondoa adha ya watoto kuandikishwa katika shule nyingine za maeneo ya mbali.


Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Aidda C. Haule, ambaye ameongoza zoezi hilo kwa kushirikiana na wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo vijana, wanawake, na hata wazee, amesema kuwa, uwepo wa shule ya sekondari katika eneo hilo, ilikuwa ni kiu ya muda mrefu, hali ambayo imewasukuma wananchi kujitokeza kwa wingi, na kujitolea kushiriki zoezi la kuchimba msingi wa shule hiyo kwa manufaa ya jamii nzima.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbalizi, Paul Mwampamba, amesema kuwa zoezi la kuchimba msingi wa shule hiyo, limekuwa shirikishi kwa wananchi wote, na kwa umoja wao wameitikia vizuri kutokana na ukweli kuwa, watoto wao wamekuwa wakilazimika kusoma katika shule ziliko mbali ikiwemo: Shule ya Sekondari Juhudi na Usongwe, hali iliyowafanya wakumbane na changamoto ya vishawishi na vihatarishi vya barabarani kutoka kwa waendesha bodaboda na bajaji.


Nae Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Usongwe, Bi. Fatma Athumani Issa, amesema kuwa, ushiriki wa wananchi katika zoezi la kuchimba msingi huo na hatua nyingine zinazokuja ni ishara nzuri ya wananchi kuonesha mshikamano kwa viongozi wao katika harakati za kuleta maendeleo muhimu katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu. Amesema mradi wa ujenzi wa shule hiyo ni utahudumia watoto wa kitongoji chote chenye wakazi takribani 41,904










Comments

Popular posts from this blog

MWENGE WA UHURU, WAZINDUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MILIONI 900. BUKOBA

MAKAMU WA RAIS, ATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA

TARURA YATENGA BIL. 1 KUKABILIANA NA EL NINO TABORA

SHULE YA MSINGI IPULI YAPEWA TUZO YA UFANISI

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUANZA JANUARI 2027

MANISPAA TABORA KULIPA MIL 27 ZA BODI YA MIKOPO