TAASISI ZA UMMA ZAAGIZWA KUJENGA VICHOMEA TAKA

 


TAASISI ZA UMMA ZAAGIZWA KUJENGA VICHOMEA TAKA  

Na Allan Kitwe, Tabora

TAASISI za umma na binafsi Mkoani Tabora zimetakiwa kutumia vichomea taka katika maeneo yao ili kuteketeza taka za kibaiolojia na kikemea na nyinginezo ili kulinda afya ya binadamu na mazingira yanayowazunguka.

Wito huo umetolewa juzi na Meneja wa Wakala wa Maabara ya Mifugo Tanzania (TVLA) Kanda ya Magharibi, Dkt. Qwari Bura, kwenye uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa kuchomea taka uliojengwa kwenye Ofisi za Maabara ya Mifugo.

Alisema kuwa mtambo huo ni maalumu kwa ajili ya kuchomea taka hatarishi hivyo taasisi zote zinapaswa kuiga mfano huo, badala ya kuteketeza taka kwa njia za kawaida ambazo ni hatarishi kwa afya ya jamii na mazingira.

Dkt. Qwari alibainisha kuwa mtambo huo una uwezo wa kuchoma hadi kilo 30 za taka ngumu na hatarishi kwa wakati mmoja.

Dkt Bura alidokeza kuwa TVLA itatoa huduma hiyo bure kwa wananchi wote wanaohitaji kuchoma taka za kibaiolojia, ila taasisi za Serikali zitatakiwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya huduma hiyo.

Kwa upande wake, Mtafiti wa Mifugo Daraja la Pili kutoka TVLA, Dikson Anjelo, alisema faida ya mtambo huo hauzalishi moshi mzito unaoweza kuathiri afya za watu wanaozunguka eneo la uchomaji taka.

Naye Daktari Mtafiti wa Mifupa kutoka TVLA, Denis Luumba, alisema uchomaji taka kwa njia za kawaida unaweza kuathiri mfumo wa upumuaji wa watu wanaohusika na zoezi hilo kutokana na moshi unaozalishwa.

Baadhi ya wananchi pia walieleza namna walivyokuwa wakikabiliwa na changamoto za kiafya na kimazingira kutokana na uchomaji wa taka kwa kutumia njia za kawaida.

 

Comments

Popular posts from this blog

RPC PWANI, AANGALIA ATHARI ZA ULISHAJI WA MIFUGO ENEO LA CHAURU.

UONGOZI WA AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YAJIDHATITI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA KUISAIDIA JAMII

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016 HAYA HAPA.

MELI YA MV CHAMBO YATEKETEA KWA MOTO.

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU KWA WASANII TOZO ZIKIPUNGUZWA

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

WAISLAMU SAADANI WAOMBA MSAADA KUJENGEWA MSIKITI.