Wednesday, May 31, 2017

SERIKALI KUENDELEA KUPAMBANA NA KILIMO CHA MIRUNGI

OTH_1290
Serikali imetangaza kuendesha operesheni ya kuteketeza mashamba ya mirungi kote nchini ikiwa ni mkakati wa kupambana na dawa za kulevya.

Hatua hiyo inafuata baada ya kuteketeza mashamba ya bangi zaidi ya 150 yenye ukubwa wa ekari 165 katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Sianga wakati akizungumza kwenye kipindi maalum kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

“Dawa za kulevya zinaathiri sana nguvu kazi ya Taifa na tangu Mamlaka hii imeanza tumefanikiwa kudhibiti uingizaji wa Heroine, Cocaine na dawa nyingine za kulevya na tumewakamata wafanyabiashara wakubwa ambao walikuwa wanatafutwa na mataifa makubwa na hiyo ni hatua kubwa kwa nchi yetu katika mapambano haya” Alisisitiza Sianga.

Akifafanua Sianga alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza kwa awamu ya kwanza kutokana na mafanikio yaliyofikiwa katika kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya na matumizi yake.

Mikoa mingine itakayofuata katika mpango wa kuanzishwa kwa vituo hivyo ni Pwani, Morogoro, Kilimanjaro na Arusha.

“Tumejipanga kudhibiti maeneo yote yanayotumika kupitisha dawa za kulevya katika hili tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ili dhamira ya Serikali ya kuondoa tatizo la dawa za kulevya hapa nchini litimie.”Alisisitiza Sianga.

Akizungumzia ushirikiano na wananchi Sianga alisema kuwa kila siku wananchi 5 hadi 10 wanafika katika Mamlaka hiyo kutoa taarifa hali inayoonyesha mwamko kwa wananchi katika kupambana na dawa za kulevya katika maeneo yao na katika Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Sianga alibainisha kuwa wameanza kufuatilia Kemikali Bashirifu zinazoingizwa hapa nchini kwa kuwa zinaweza kutumika vibaya na watu wenye nia mbaya kuzalisha dawa za kulevya.

“Kemikali Bashirifu zinaweza kutumika vibaya kuzalisha dawa za kulevya hivyo lazima tuzifuatilie na kudhibiti uingizwaji wake ili uzingatie sheria na taratibu na zitumike kwa makusudi chanya tu na si vinginevyo.” Alieleza Sianga.

Hivi karibuni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini,kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA,walifanikiwa kukamata shehena kubwa ya kemikali Bashirifu zinazoweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya katika eneo la Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Aidha katika msako huo pia mfanyabiashara Benedict Assey mmiliki wa shehena hiyo alibainika kumiliki kiasi kikubwa cha kemikali hizo katika Miji ya Bagamoyo,na Moshi mkoani Kilimanjaro.

TAARIFA KWA WAKAZI WA WILAYA YA BAGAMOYO.

IGP SIRRO AANZA KUSHUGHULIKIA MAUAJI MKOANI PWANI.

1
Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za  kudhibiti masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es Salaam.
34
Sehemu ya waandishi wa habari pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza IGP Mpya, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam
............................
Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro ameahidi kutoa sh.milion 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya viongozi huko Kibiti wilayani Rufiji Utete mkoani Pwani.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kumekuwa na mauaji ya wananchi na Askari katika Wilaya ya Rufiji Utete pamoja na Wilaya ya Mkuranga ambayo yamekuwa yakifanywa na wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao.

Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na Operesheni mbalimbali kuhakikisha kwamba vitendo hivyo haviendelei kuweza kubaini mzizi.

Aidha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mpya amezungumzia juu ya waendesha boda boda kuwa na tabia ya kukaidi kufata sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja ‘mishikaki.

Sirro amesema waendesha bodaboda wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kupita taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu ‘Helment’ ambapo kumesababisha wengine vifo na majeruhi ya kuwafanya kuwa na ulemavu wa kudumu.

Hata hivyo amesema kumekuwa na malalalamiko dhidi ya baadhi ya Askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa lakini pia baadhi ya wananchi kuwashawishi Askari kupokea rushwa ikiwa ni sehemu ya ngao ya kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa wamefanya makosa.

MAGAZETI YA LEO 31 MAY 2017.

Thursday, May 25, 2017

WAHARIRI HABARI WAPEWA SEMINA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.
 
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Wakili Harold Sungusia akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada anuai.
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Robart Zephania (mbele aliyesimama) akizungumza katika semina hiyo.