Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa
kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo,
Dk. Hedwiga Swai.
............................................
WANANCHI
wametakiwa kupima kila wakati na kuendelea kutumia kinga ili kujiepusha na
maambuki mapya ya VVU.
Mwito huo
umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika kikao cha makamishina wapya wa tume hiyo
kilichoketi jijini Dar es Salaam juzi.
“Tunapaswa
kuwa ni mikakati endelevu ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwani bado
kunachangamoto kubwa” alisema Maboko.
Maboko
alisema watanzania wasidanganyike kuwa ukimwi umekwisha ugonjwa huo bado upo na
ni changamoto kubwa.
Alisema
changamoto kubwa ya ugonjwa huo bado ipo katika baadhi ya mikoa hasa ile ya
nyanda za juu kama Iringa na Njombe hivyo wananchi wasibweteke kuwa ugonjwa huo
umekwisha.
Alisema
kwa Tanzania Bara kunamaambukizi ya asilimia 5.3 sawa na watu milioni mbili
waliopata maambukizi.
No comments:
Post a Comment