Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa
Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi wa
Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo
Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally
Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba,
Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
.............................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi
Magomeni watumie utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa wakati.
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati alipokagua ujenzi wa
nyumba hizo zinazojengwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amewataka wataalamu hao waendelee kufanya kazi hiyo kwa kufuata misingi ya
weledi wa taalauma yao kwani Serikali inawaamini.
“Muhimu mjue kwamba mmepewa
dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili wananchi waliokuwa wanaishi
hapa waweze kurudi katika makazi yao,” amesema.
Kwa
upande wake,
Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Mhandisi Edwin Nnunduma amesema awamu ya kwanza
ya ujenzi huo itahusisha majengo matano ya makazi. “Kati ya majengo haya
matano, manne yatakuwa na ghorofa nane na moja litakuwa na ghorofa tisa, ambapo
wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wanaishi eneo hili tangu zamani watakabidhiwa,”
amesema.
Mhandisi
Nnunduma amesema majengo hayo yanajengwa kwa teknolojia ambayo imezingatia
uwezo wa wakazi wake ambapo ina majiko yanayoweza kutumia kuni na mkaa.
Amesema
mradi huo ambao unajengwa kwa awamu tofauti utahusisha ujenzi wa nyumba za
makazi, maduka makubwa na ya kisasa pamoja na ofisi.
Mhandisi
huyo amesema awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba Mosi, mwaka huu inahusisha ujenzi
wa nyumba za makazi ya wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo ambayo
inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana
na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini
Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa
Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma kuhusu Mradi wa Ujenzi wa
Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo
Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya WaziriMkuu)
No comments:
Post a Comment