Bonanza la
michezo liliofanyika jana Tarehe 27 Novemba, katika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini, limejumuisha
timu 11 kutoka Dar es slaam na Pwani na
kulifanya liwe kivutio cha aina
yake pale timu za maveterani zilipomenyana
vikali katika kuonyeshana uwezo.
Katika michezo hiyo timu ya Halmashauri ya
Bagamoyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Kilungule, Timu
ya Mapinga ilichuana na Neibour ambapo
Neibour ilitoka na ushindi wa bao 1 na Mapinga haikupata kitu.
Aidha katika Mechi nyingine Mapinga ilicheza na
Temboni ambapo Temboni waliichapa
Mapinga bao 1-0, Timu ya Mwenge Veterani imeilaza Timu ya
Leaders mabao 2-0, huku Corner ikwa imeichapa Kibamba mabao 2-0, na Kibaoni
imeibuka na ushindi wa bao 1 dhidi ya Golan ambayo haikupata kitu.
Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza hilo, Deodatus
Katambi alisema Bonanza hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa
matarajio yalikuwa ni kuwa na timu 6 lakini zimepatikana timu 11
zilizoshiriki katika michezo hiyo.
Alisema watu wanapenda Michezo bila ya kujali umri wao na kwamba kinachokosekana ni
kumpata mtu wa kuwaunganisha pamoja ili waweze
kuonyesha uwezo wao.
Katambi ambae ni katibu wa Temboni Veterani ambao
ndio walioandaa Bonanza hilo, alisema timu zote zilionyesha uwezo mzuri na
kupelekea ushindani kuwa mkubwa jambo ambalo liliwavutia watazamaji.
Aliongeza kwa kusema kuwa, timu ya Halmashauri ya
Bagamoyo ilikuwa vizuri katika mchezo na kutoa wito kwa serikali kuzijengea
uwezo timu za Halmashauri ili kupata timu bora itakayoleta burudani katika
sherehe mbalimbali na kuwajengea afya
bora kutokana na mazoezi.
Mechi hizo zilizochezwa katika uwanja wa
mwanakalenge mjini Bagamoyo zilichezeshwa na waamuzi Raphael Ntasi, Idi Mpingo, Jafari Shaweji, wengine ni
Hamadi Kidodi, Shabani Milao na Mohamedi Toloa.
Wachezaji
wa timu ya Temboni veterani wakiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya pambano lao
na Mapinga Veterani, katika Bonanza la michezo lililofanyika uwanja wa
Mwanakalenge Bagamoyo mjini.
Nyama choma, vinywaji na vyakula vilipatikana katika Bonanza hilo
Wachezaji
pamoja na watazamaji wakiwa wametulia kufuatilia michezo iliyokuwa ikiendelea
Mratibu
m kuu wa Bonanza hilo kutoka Tembeni Veterani, Deodatus Katambi akizungumza na
waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment