Mwenyekiti
wa Chama cha Waigizaji mkoani Mwanza, Ramadhan Mustapha (kushoto), akipokea
cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha,
aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii
wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
.................................
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary
Tesha, amemtaka Afisa Utamaduni mkoani mkoani hapa, kuhakikisha maadhimio
yaliyoafikiwa na wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza yanaanza hatua za utekelezaji
ndani ya siku saba.
Nje ya hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Tesha
amesema Afisa Utamaduni mkoa wa Mwanza, James Willium, kwa kushirikiana na
maafisa utamaduni wa halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha
wanatoa mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye mafunzo hayo
ili utekelezaji huo uanze mara moja.
Miongoni mwa maadhimio saba ya wasanii walioshiriki
mafunzo hayo ambayo yamewasilishwa na Mwakilishi kutoka Chama cha
Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela, ni pamoja na uongozi
(Serikali) wa mkoa wa Mwanza kusaidia upatikanaji wa kituo cha sanaa (studio ya
kisasa) kwa ajili ya kurekodia filamu na vipindi vya runinga pamoja na
kushirikishwa kwenye dhifa mbalimbali za kimkoa na kitaifa ili kuonesha kazi
sanaa zao.
Katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya
Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa, ametoa bure kiwanja chenye ukubwa
wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza ili wasanii wa filamu mkoani
Mwanza wajengewe studio kwa ajili ya kurekodia kazi zao ambapo Mfuko wa
Pensheni wa PPF umeonesha nia ya dhati ya kufadhiri ujenzi wake.
Zaidi ya washiriki 300 wamepata mafunzo hayo
ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema yamelenga
kuwajengea weledi wadau wa filamu wakiwemo waigizaji, waongozaji na wahariri,
kutengeneza kazi zenye ubora, kutambua majukumu ya bodi hiyo, hakimili na
hakishirikishi ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea
cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce
Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu mkoani
Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba 12,2016 katika
ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa
wa Mwanza, John Mongella.
Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy
(kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo
kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto), akipokea cheti cha
utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa
mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani
Mwanza hii leo.
Mwakilishi
kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela
(kushoto), akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Mary Tesha.
Mshauri
wa sanaa ya Filamu mkoani Mwanza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti
wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Washiriki
wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza wakifuatilia burudani kutoka kwa msanii wa
nyimbo za asili, Chifu Mwananzengo kutoka wilayani Kwimba hii leo.
Washiriki
wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo hii
leo kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
Washiriki
wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kutoka kwa Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso.
Washiriki wakiwa katika Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment