Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi
akiongea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
.........................................
BARAZA la Madiwani Wilayani Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi
wawili wa Halmashauri hiyo kutokanana makosa ya wizi wa mamillioni ya fedha za
wafadhili za mradi wa UKIMWI wa Water Reed
Akizungumza wakati wa kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo
mara baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na kamati ya uchunguzi
iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la pili Josephat
Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya zaidi Milioni
84.
“Josephati aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200
/-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha
shilingi milioni 48742500/-fedha za mradiwa Water Aid zilizofika katika
Halmashauri ya wilaya ya Ileje”alisema Songa
Mwenyekiti huyo ameagiza watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha
katika Akaunti ya Halmashauri hili ziweze kufanya kazi zingine.
Kwa mtumishi mwengine Anna mwakipesile kesi yake bado inaendelea na
uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras
wa mkoa wa Songwe waliachiwa huru na kurudishwa kazini baada ya tume kuridhika
na utetezi wao
Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa
shule wawili ambao ni Henry Musomba wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa
sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu
na matumizi mabaya ralislimali
Aidha Mnasi alisema kuwa ni wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini
kujitathimni kwa kile alichofanya kwani waliotuhumiwa ni wengi lakini bado
uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo kwani kila mmoja atakayebainika
kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.
Ametoa onyo kwa watumishi kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na
maadili ya utumishi wa kwa kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali
aitamfumbiamcaho kwani hu ni wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa
maslahii ya Taifa
“Mimi sipo tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe
nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi
kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli” alisema Mnasi
Sehemu
ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
No comments:
Post a Comment