Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, wa kushoto akiwa na Afisa Mtendaji wa Shirika lisilo la
kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr
Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, wa pili kutoka kushoto anayemfatia ni Afisa Mtendaji Bw.Nasr Al
Jahdhamy mwakilishi kutoka Oman na Katibu wa Mbunge Bwana Iddi Swala na Mzee Maokola
wakati wa kukabidhi visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete, akiongea na wananchi wa jimbo hilo akiwa na Afisa Mtendaji
wa Shirika lisilo la kiserikali toka Nchini Omani linaloitwa
TUELEKEZANE PEPONI Bw.Nasr Al Jahdhamy wakati wa kukabidhi
visima vitatu kwa wananchi wa jimbo hilo.
.................................
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa visima Vitatu
vyenye thamani ya Shilingi Milioni 48.5 toka kwa Shirika lisilo la
kiserikali toka Nchini Omani linaitwa kwa TUELEKEZANE
PEPONI chini ya Afisa Mtendaji wake Nasr Al Jahdhamy.
Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo Mbunge huyo alisema
kuwa , shida ya maji ndani ya Halmashauri ya chalinze imekuwa kubwa na kueleza
kuwa kazi iliyofanyika kufanikisha ujenzi wa visima hivyo ni kubwa ili kusaidia
tatizo hilo kwa kipindi hiki wakati wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi
wa kutoa maji mto wami.
“Nimeona nifanye kazi ya kutengeneza visima ili kupunguza ukali wa uhaba
wa maji kwani matengenezo ya mradi wa wami bado yanaendelea kuchimbwa kwa
visima hivi si ishara kuwa ule mradi wa maji ambao tuliongea kuwa umekufa mradi
wa wami utakapokamilika tunataraji utawanufaisha wananchi wengi wa jimbo
letu.”alisema Ridhiwani
Aidha visima hivyo vitatu vimekabidhiwa katika kijiji cha
matipwili , shule ya sekondari ya matipwili na kijiji cha Gongo ambavyo
vinaendelea kujengwa na vinataraji kukamilika mapema ndani ya wiki ijayo.
Naye Bwana Naseer aliahidi kuendelea kumsaidia Mbunge kufikia malengo
yake ya kusaidia kutatua changamoto zinazokabili nyimbo hilo,na kuongeza kuwa
atasaidia kuchimba visima vingine kumi katika Halmashauri hiyo na
kusaidia michezo.
No comments:
Post a Comment