Monday, November 7, 2016

RC. PWANI AMPONGEZA DC BAGAMOYO KWA KUTEMBELEA MAENEO YAKE NA KUWATAKA VIONGOZI WENGINE MKOANI PWANI KUIGA MFANO.


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mhandisi Everist Ndikilo akizungumza na waandishi wa habari shule ya msingi Kibindu katika Halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaji, Majid Mwanga.
 ...........................................


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist  Ndikilo, amempongeza mkuuwa wa wilaya ya  Bagamoyo Majid Mwanga kwa kutembelea maeneo yake na kubaini changamoto mbalimbali.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea kata ya Kibindu wilayani Bagamoyo ambapo alikuta ujenzi  wa madarasa ukiendelea huku ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga.

Aidha, amewataka viongozi wote wa serikali mkoani Pwani kuacha kukaa ofisini pekee na badala yake watembelee maeneo yao ili kujionea changamoto zilizopo kwenye maeneo mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi.

Alisema kitendo cha  mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kutembelea maeneo yake kimepelekea kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa katika baadhiya shule nahivyo ameweza kuchukua hatua ya kuona namna gani changamoto hiyo inaweza kutatuliwa.

Alimpongeza pia Diwani wa kata ya Kibindu, Mkufya Ramadhani Mawazo, Mwenyekiti wa kijijicha Kibindu, Yusuf Mahimbo na Afisa Mtendaji kata ya Kibindu, Godwin Mhagama kwa kushirikiana vyema katika kuwahamasisha wananchi kushiriki ujenzi wa huo wa madarasa.
Akizungumzia hali hiyo, mwenyekiti wa kijiji cha Kibindu, alisema wamefanikiwa kwa kuwashirikisha wananchi kila hatua hali ilyopelekea wananchi kujitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo.


Alisema wameweka utaratibu  wa  kila siku wanapatikana wananchi wa kitongoji  kimoja ili kushiriki shughuli hiyo ya maendeleo ambapo hiyo inatoa nafasi kwa vitongoji vingine kujiandaa kwaajili ya siku yao.
Akielezea hali hiyo, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, alisema amefikia uamuzi wa kuweka kambi katika shule hiyo ili kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa,  ambapo  inaupungufu wa vyumba vyamadarasa.

Alisema tatizo  la madawati katika shule za wilaya ya Bagamoyo  limekwisha  na  kwamb a kilichobaki sasa ni kuongeza idadi ya vyumba vya  madarasa katika baadhi ya shule na kuanzisha shule mpya katika maeneo ambayo hakuna shule ili kuwaondolea watoto adha ya kutembea umb ali mrefu kufuata shule hali inayopelekea kuchoka.


Akiilezea shule ya msingi Kibindu alisema, shule hiyo ina wototo zaidi ya elfu moja wakati vyumba vya madarasa ni vinne tu ambapo watoto hulazimika kukaa chini kwa sababu ya hakuna nafasi ya  kuweka madawati.

Aliongeza kwa kuwataka wadau mbalimbali kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika maeneo yenye mahitaji ili kuisadia serikali katika kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika jamiii.

Wananchi mbalimbali walioongea na bagamoyokwanza blog. walisema wamefarijika na kitendo cha mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kukaa na wao  kwa  muda wa siku nne  huku  akishiriki kazi za ujenzi kama mwananchi wa kawaida.

Walisema hawajawi kuona mkuu wa wilaya kufika katika kijiji hicho na kukaa nae hivyo kitendo cha mkuu wa wilaya wa sasa Majid Mwanga ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine katika kuwa karibu na wananchiili kujua  matatizo yanayowakabili katika huduma mbalimbali.
Wananchi wakichanganya  Zege kwenye  ujenzi huo.

Watumishi mbalimbali katika Halmashauri ya  chalinze  wakijipanga mstari  kwaajili ya kubeba zege kwenyeujenzi huo, mwenye fulana ya bluu na  kilemba ni  Afisa mtendaji wa kata ya Mbwewe, Elizabeth Msenga, anaefuatia kulia ni Afisa kilimo kata ya Mbwewe, Prinscus Mrina.

Mwenye fulana ya njano na kilemba ni Afisa tarafa kwa ruhombo, Renitha Ruzabico akishiriki  katika ubebaji zege  kwenye ujenzi wa madarasa shule ya msingi Kibindu


Diwani  wa kata ya Kibindu,Mkufya Ramadhani  Mawazo mwenye fulana nyeusi na mistari meupeakiwa katika umwagaji wa zege kwenye ujenzi huo.
Mkuu wa  wilaya ya  Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga  akiwa juu ya  jengo kwaajili ya kumwaga zege.


Baada ya  mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid  Mwanga , kuweka kambi kwa  muda wa  siku nne, jengo la vyumba  viwili vya  madarasa limefikia hivi.

No comments:

Post a Comment