Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani, ambayo kitaifa
yalitarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam,Desemba 3, mwaka huu yameahirishwa
na badala yake kila mkoa utaadhimisha kivyake.
Akitoa tamko la kuharishwa kwa maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene
amesema maadhimisho hayo yalilenga kila halmashauri isafirishe wanachama wa
vyama vya watu wenye ulemavu ili washiriki maadhimisho hayo jijini humo.
Amesema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kwa wakuu wa mikoa kuwa badala ya maadhimisho hayo ya kitaifa kukusanya
walemavu wote kwenye mikoa kwenda Dar es salaam yafanyike kwenye mikoa yao.
No comments:
Post a Comment