Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majid Mwanga, akikabidhi shilingi
laki moja kwa kikundi cha Bodaboda
Mapinga, mara baada ya kuzungumza nao.
......................................
Mkuu wa wilayaya Bagamoyo ametoa elimu kwa
waendesha Bodaboda wa kata ya Mapinga na kuwataka waache kufanya urafiki wa
kimapenzi na wanafunzi ili kuwapa nafasi ya kuendelea kimasomo.
Mkuu huyo wa wilaya amesema wanafunziwengi
wasichana hutumia usafiri wa bodaboda kufika shuleni ambapo madereva wa
bodaboda hutumia nafasi hiyo kuwalaghai kimapenzi hali inayopelekea wanafunzi
kukatisha masomo kwa kupata mimba na
vishawishi vingine.
Alisema jamii inahitaji kina mama walioenda shule
ili kusimamia vyema majukumu yao na kwamba kina mama wanaotarajiwa ni hawawasichana wa sasa ambao wanakumbana na
changamoto za waendesha bodaboda.
Aidha, aliwataka kutoa ushirikiano kuwafichua
wale wote wenye tabia hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Mkuu huyo
wa wilaya aliwachangia shilingi laki moja waendesha boda boda hao katika
kikundi chao ikiwa ni ishara ya kutambua mchango
wao katika jamii katika kazi wanazofanya huku akiwasihi
kutovunja sheria za nchi.
Waendesha bodabodaMapinga wakimsikiliza mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo mara alipowatembelea na
kuzungumza nao.
No comments:
Post a Comment