Katibu
Msaidizi toka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja
Masesa akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam
kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wa Umma wanazingatia
maadili ya Utumishi wa Umma ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.
........................................
Serikali imewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi wa
Umma ili kuleta ustawi kwa wananchi kwa kutekeleza mipango inayolenga
kukuza uchumi na kutoa huduma bora.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Msaidizi kutoka
Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa wakati wa mkutano na
vyombo vya Habari.
Bw. Masesa amesema kuwa Matokeo ya Makosa ya watumishi wa Umma waliokata
rufaa Tume ya Utumishi wa Umma mwaka 2014/2015 yanaonyesha kuwa kati ya
watumishi 135 walikata rufaa walipatikana na makosambalimbali ambapo 54
walipatikana na kosa la utoro kazini.
Bw. Masesa aliongeza kuwa watumishi wengine 16 walishindwa kutekeleza
majukumu yao,10 kumdharau mwajiri,8 kughushi nyaraka mbalimbali,8 kufanya
malipo kinyume na taratibu,aidha makosa mengine yalikuwa chini ya watumishi 7.
Aidha Masesa aliwataka watumishi wa Umma kujiepusha na vitendo vya
rushwa,ulevi,utoro makazini na matendo yote yanayokwenda kinyume na maadili ya
utumishi wa umma.
“ Utendaji kazi katika utumishi wa Umma huongozwa na
sheria,kanuni,taratibu na Miongozo mbalimbali ambayo ipo”Alisisitiza Masesa.
Pia Masesa amesema kuwa watumishi watakaoshindwa kuzingatia
taratibu zilizowekwa watachukuliwa hatua kali za kisheria na mamlaka za nidhamu
katika taasisi husika.
Tume ya Utumishi wa Umma,inawataka waajiri,Mamlaka za ajira na nidhamu na
Watumishi wote kuzingatia kanuni za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu
yao ili kukuza uchumi,kutoa huduma bora kwa jamii na kulinda amani na utulivu
wan chi.
Katibu
Msaidizi toka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi
akisisistiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es
salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari. Kulia ni Katibu msaidizi wa Tume
hiyo Bw. Peleleja Masele,kushoto ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Tume hiyo Bi
Jorlin Kagaruki.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi
wa Umma uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment