Waziri wa viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh.
Charles Mwijage leo tarehe 16 Novemba 2016 ametembelea ujenzi wa viwanda viwili
katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Waaziri Mwijage alikuwa na ziara mkoani Pwani amb
apo katika wilaya ya Bagamoyo alitembelea viwanda viwili, ambavyo ni kiwanda
cha juisi cha Sayona kinachojengwa kijiji cha Mboga kata ya Msoga Halmashauri
ya Chalinze na kiwanda cha kukausha matunda mbalimbali kwaajili ya soko la nje
cha Elven Agry, kilichopokata ya Mapinga Halmashauri ya Bagamoyo.
Aidha, amewataka wananchi wa maeneo hayo
kuwapeleka shule watoto wao ili waingie kwenye ushindani wa soko la ajira
katika viwanda hivyo.
Aliongeza kwa kuipongeza kampuniya Sayona kwa
kuwadhamini vijana kutoka eneo la Msoga kwenda kusoma ili waje kupata ajira
katika kiwanda hicho.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi msadizi wa Sayona
Group, Aboubakari Mlawa, wa kulia, kushoto ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid
Mwanga.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, katikati, Charles Mwijage akielezea jambo
katika kiwanda cha Juisi cha Sayona kijiji cha Mboga kata ya Msoga Halmashauri
ya Chalinze.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, katikati, Charles Mwijage akielezea jambo
katika kiwanda cha Juisi cha Sayona kijiji cha Mboga kata ya Msoga Halmashauri
ya Chalinze anaesikiliza mwenye shati jeupe ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Almasi Masukuzi.
Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakipiga
picha ya pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katika kiwanda cha Sayona kilichopo kata ya Msoga.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha kukausha matunda, Mr.
Darpan kiwanda kilichopo kata ya Mapinga Halmashauri ya Bagamoyo
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akifafanua jambokwa Mkurugenzi
wa kiwanda cha kukausha
matunda kilichopo mapinga, kulia ni mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy
Aliy akimtambulisha Waziri wa
Viwanda kwa madiwani wa kata ya Mapinga Ibrahim Mbonde na Diwani wa kata ya Dunda, Dickson Makamba.
Muonekano wa ujenzi wa kiwanda cha kukausha
Matunda cha Elven kilichopo kata ya
Mapinga Bagamoyo
No comments:
Post a Comment