Tuesday, November 15, 2016

BARAZA LA MADIWANI BAGAMOYO LAKATAA TAARIFA ZA KATA 5 KUTOKANA NA MAPUNGUFA YA UANDAAJI.

Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauriya Bagamoyo, Aliy Aliy na makamo mwenyekiti, Mohamedi Usinga wakimsikiliza Diwani wa kata ya Magomeni, Mwanaharusi Jarufu.
.................................
 
Baraza  la Madiwani la Halmashauri ya Bagamoyo limekataa Taarifa tano za maendeleo ya kata zilizowasilishwa katika kikao hicho.

Akizungumza katika kikao cha robo ya  kwanza 2016/2017 mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo Aliy Aliy, alisema wamefikia uamuzi huo wa kuktaa taarifa hizo ili kutoa fundisho  kwa watendaji kata ambao wanaandaa taarifa hizo.

Mwenyekiti huyo ambae ni Diwani wa  kata ya Fukayosi  alisema Taarifa iliyoanza kuwasilishwa ni ya kata yake hivyo alikuwa wa kwanza kuikataa kwakuwa inamapungufu, na kuwataka madiwa ambao taarifa zao zinamapungufu hawana budi kukubali makosa hayo na kurudi kurekebisha ili kumbukumbu zitakzohifadhiwa katika ofisi ya Halmashauri ziwe sahii.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Bagamoyo, aliwataka watendaji kata kuacha kufanya  kazi kwa mazoea na badala yake waongeze ufanisi katika utekelezaji ili kwenda sambamba  na kauli mbiu ya Rais Dkt. John Magufuli ya hapa kazi tu.

Aidha, aliwataka madiwani kufanya vikaona kuridhia taarifa zinazoandaliwa na watendaji na kurekebisha mapema  mapungufu ili kutoa fursa  kwa baraza kujadili mambo mengine na kuongeza kuwa si vyema kusaini taarifa ya maendeleo bila ya kuipitia kwa kufanya hivyo unaweza kusaini taarifa yenye  mapungufu.

Mwenyekiti huyo huyowa Halmashauri aliwataka watendaji kuacha  kufanya kazi kwa mazoea  na badala wafanye kazi kitaalamu kwa uwajibikaji wa hali ya juu ili kufikia malengo waliojiwekea.

Kata ambazo zimekataliwa taarifa  zake kutakiwa kuzirekebisha ni  Kata ya Magomeni, Nianjema, Kerege, Kiromo na  Kisutu
Taarifa za kata zinapaswa kuwasilishwa kwenye kikao cha baraza la  madiwani ili kuainisha  Taarifa za kata  ikiwemo idadi ya watu,kaya zilizopo, hali uchumi katika kata na vyanzo vya mapato.










1 comment:

  1. Tunashukuru kwa taarifa ya hapa Nazi.mwandishi asante kwa kutujusha habari,ingipendeza zaidi kwa Sikh za usoni kuelezea zaidi sababu za kuzikataa hizo taarifa nini mapungufu yake je ni uzembee,ukiuwaji was taratibu au mini kuliko kuishia mapungufu mapungufu gani??????

    ReplyDelete