Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge.
............................................
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la
Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa
ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni
ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya
kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko
kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee,
waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo
wa kupita hapo.
Hii ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”,
kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa
jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono
jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni
nyingine wajifunze katika hili.
Katika uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza
kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo
ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za
kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya
Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate
huduma bora za ijamii.
Akiwasilisha kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Zaituni
Marunda amesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya
ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado
hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa
na wawekezaji.
Aidha Neema John aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo
wamekuwa wakisumbuliwa na kero za maji, umeme na Zahanati hivyo wameiomba
Serikali iwasaidie kutatua kero hizo znazowaathiri zaidi kinamama ambao
hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji pamoja na kupata taabu wakati
wa kujifungua.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi
kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze
kushughulikia kero na pia aliweza kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata
kwa kuchangia Bati 100 na kuungwa mkono na Bw. Hans Paul aliyetoa
matofali 5000 huku Bw. Jagjit Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200 na
Mkurugenzi wa Jiji Bw. Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa zahanati
hiyo.
Daraja la Mto kijenge lilioanza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost
2016 lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani
tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza kudumu
kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .
Diwani
wa Kata ya Engutoto kwa kupita Tiket ya Chadema Aman Reward alishirki
katika uzinduzi wa Daraja na kupongeza Viongozi wa Mkoa na Jiji kwa
namna wanavyowatumika wananchi.
Diwani
wa Kata ya jirani ya Themi kupitia Tiketi ya Chadema Melance Kinabo pia
alishirki katika uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa
mwananchi kama zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa Unzinduzi wa Daraja
la Mto Kijenge.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kata ya Engutoto
na Moshono wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.
Mkuu
wa wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa
maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) na Bw. Jagjit Aggarwal.
Daraja
walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja
la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul
Hili
ndilo Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa
Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita
2.2 na uwezo wa kudumu kwa miaka 50.
No comments:
Post a Comment