Tuesday, November 1, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA NAIROBI SOUTHERN BYPASS KATIKA ENEO LA KAREN NCHINI KENYA

kiny3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
 kiny7

Sehemu ya barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
 kiny4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Karen nchini Kenya mara baada ya kufungua barabara ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya. 
 kiny2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa mara baada ya kuwasili katika eneo la Karen jijini Nairobi.
 kiny8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakicheza wimbo pamoja na kikundi cha kwaya katika eneo la Karen mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
 kiny9

No comments:

Post a Comment