Sunday, November 27, 2016

DC BAGAMOYO APOKEA SARIJI MIFUKO 400 KUTOKA NYATI CEMENT KWAAJILI YA UJENZI WA MADARASA.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, akipokea mifuko 400 ya Saruji kutoka Nyati Cement, kwaajili ya ujenzi wa  vyumba  vya madarasa anayemkabidhi katikati ni makamo wa rais wa kampuni ya Nyati Cementi, Mr Pathank,  wanaoshuhudia kulia ni meneja wa masoko, Mr, Mahesh Batt, upande wa kulia mwenye miwanini Mwenyekiti wa Halmashuri ya Bagamoyo, Aliy aliy, anafuata ni Mkurugenzi wa Halmashuri ya Bagamoyo, Fatuma Omari Latu.
 ............................................
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid mwanga amepokea Saruji mifuko mia nne kutoka kwa Nyati Cementi kwaajili ya ujenziwa Madarasa katika wilaya hiyo.

Akipokea msaada huo wa Saruji Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru  wadau hao ambao wameahidi kusaidia mifuko 800 ambapo wameanza kwa kukabidhi mifuko 400.

Amesema maendeleo katika jamii yanaletwa kwa ushirikiano katiya serikali  na wananchi kwa kusaidiwa na wadau mbalimbali  katika kufanikisha mahitaji muhimu.

Aliongeza kuwa wilaya ya  Bagamoyo kwa imekamilisha utengenezaji wa madawati na hivyo  kufikia  lengo  la utenegenezaji wa  madawati lakini changamoto  iliyopo  ni  upungufu  wa vyumba vya madarasa.

Alisema kwa kutumia Saruji hiyo, itasaidia kuongeza nguvu  katika maeneo ambayo ujenzi wa madarasa unaendelea.

Aidha,alisema kuwa kata zitakazofaidika na Saruji hiyo  ni zile ambazo  tayari zimeanza ujen zi na kwamba watapata saruji hiyo  kwaajili ya umaliziaji tu.

Nae meneja  wa masoko wa Nyati Cement, Mahesh Batt,  amesema kuwa kampuni yake  imejipanga  kuwekeza katika wilaya ya Bagamoyo ambapo inatarajia  kujenga  kiwanda cha  Saruji  katika eneo  la Talawanda  wilayani hapa ili kutoa fusa ya ajira  na kusogeza huduma ya bidhaa hiyo kwa mikoa ya  Morogoro, Dodoma, Tanga na Pwani.

Kwa upande wake  mwenyekiti  wa  Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy amepongeza mkuu  wa wilaya ya  bagamoyo  kwa kuunganisha  wadau  mbalimbali  katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuahidikutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda cha Saruji  katika eneo la  Talawanda.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kugawana halmashauri bado wilaya ya Bagamoyo ni moja na kwamba atashirikiana na mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze ili kuhakikisha Kiwanda  hicho  kinajengwa katika eneo  la Talawanda.






No comments:

Post a Comment