TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba
26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC Jaji
Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na
sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu,
kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza
kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za
mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43
zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha kwamba
kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292
kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume
kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea
taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya
Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina
wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii
kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe
26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa
uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na
kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.
Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa,
Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye
uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na
Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya
Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka
2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na
maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi
mdogo.
Kata ambazo zitashiriki kwenye
uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika
katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:
Na
|
MKOA
|
HALMASHAURI
|
KATA
|
1.
|
ARUSHA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
|
Musa
|
Halmashauri ya Jiji la Arusha
|
Muriet
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Ambureni
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Ngabobo
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Maroroni
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Leguruki
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
|
Makiba
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
|
Moita
|
||
2. 2
|
DAR ES SALAAM
|
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
|
Mbweni
|
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
|
Kijichi
|
||
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
|
Saranga
|
||
3.
|
DODOMA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
|
Chipogolo
|
4.
|
GEITA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale
|
Bukwimba
|
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
|
Senga
|
||
5.
|
IRINGA
|
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
|
Kitwiru
|
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
|
Kimala
|
||
6.
|
KILIMANJARO
|
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
|
Bomambuzi
|
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Mnadani
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Machame Magharibi
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
|
Weruweru
|
||
7.
|
LINDI
|
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
|
Chikonji
|
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
|
Mnacho
|
||
8.
|
MANYARA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’
|
Nangwa
|
9.
|
MBEYA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
|
Ibighi
|
10.
|
MOROGORO
|
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
|
Kiloka
|
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
|
Sofi
|
||
11.
|
MTWARA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
|
Milongodi
|
Halmashauri ya Manispaa ya
Mtwara Mikindani
|
Reli
|
||
Halmashauri ya Mji wa Masasi
|
Chanikanguo
|
||
12.
|
MWANZA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
|
Kijima
|
Halmashauri ya Jiji la Mwanza
|
Mhandu
|
||
13.
|
RUKWA
|
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
|
Sumbawanga
|
14. 14
|
RUVUMA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
|
Lukumbule
|
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
|
Kalulu
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
|
Muongozi
|
||
15.
|
SINGIDA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
|
Siuyu
|
16.
|
SIMIYU
|
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
|
Nyabubinza
|
17.
|
SONGWE
|
Halmashauri ya Wilaya ya Momba
|
Ndalambo
|
18.
|
TABORA
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
|
Nata
|
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
|
Muungano
|
||
19.
|
TANGA
|
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
|
Majengo
|
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto
|
Lukuza
|
||
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
|
Mamba
|
Imetolewa
leo tarehe 04 Oktoba, 2017.
No comments:
Post a Comment