Monday, October 9, 2017

ABDUL SHARIFU ZAHORO, MWENYEKITI MPYA WA CCM BAGAMOYO.

Mwenyekiti Mpya wa CCM Wialaya ya Bagamoyo, alhaj Abdul Sharif Zahoro akiwa amepokelewa kata ya Kisutu, Mjini Bagamoyo.
 ............................................

MWENYEKITI mpya wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo ,alhaj Abdulsharif Zahoro ,amesema atahakikisha anasimamia mali na vitega uchumi vya chama ili kiweze kujitegemea na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba.


Aidha amedhamiria kwa dhati kukipigania chama kivitendo ,kufuatilia utekelezaji wa ilani kwenye ,mashina,matawi,kata na halmashauri ili kuweka njia nyepesi ya ushindi katika chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 .

Pamoja na hayo ,alhaj Abdulsharif ,amewataka wenyeviti wa vitongoji,madiwani na wabunge wilayani humo ,kutumia dhamana na nafasi walizochaguliwa kutekeleza ahadi walizozitoa  kwa wananchi kabla ya kusubiria kukaribia kwa uchaguzi .

Aliyasema hayo ,wakati alipo pokelewa na wanachama wilayani Bagamoyo,kata ya Kisutu ,ambapo ndipo alipozaliwa na kukomaa kisiasa ,baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo kwa kupata kura 711.

Abdulsharif aliomba ushirikiano kwa wanachama ,viongozi kuanzia ngazi za chini na ambao kura hazikutosha kumuunga mkono ili kuimarisha chama kiweze kusonga mbele .

Mwenyekiti huyo ,alieleza CCM wilayani humo ina mali zake hivyo ni jukumu lake kufuatilia mapato na kuinua zile ambazo zinaonekana zinayumba kimapato .

Alhaj Abdulsharif alisema kuwa,haiwezekani vibanda vya biashara ambavyo vipo chini ya chama wilaya vikalipa fedha kwa kutumia njia zisizo kwenye maandishi ,suala ambalo atahakikisha analifuatilia ili kuongeza mapato na chama kiweze kujiendesha .

“Chama hiki kina vitega uchumi vingi ,na hizi hizi zinaweza kutuvusha kwenye hii hali ya kutembeza kibakuli kuombaomba ,tunapaswa kupigania vitega uchumi vyetu tujikomboe “

“Mie sijaja kufuata fedha ndani ya chama ,ninachotaka chama kijikwamue kiuchumi na tusimamie kwa umoja wetu ilani kwa lengo la kuendelea kushika dola ” alifafanua alhaj Abdulsharif .

Hata hivyo ,alisema kila mmoja atabeba mzigo wake kwani ambae atabainika kufanya ubadhilifu kwenye mali za chama hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake .

Alhaj Abdulsharif alizitaka,halmashauri zitekeleze ilani kwa kuboresha huduma za kijamii .

“Nitafuatilia ,tusimamie ilani na wataalamu ,kwani kuna mambo yapo sawa na mengine hayajakaa vizuri sana ,tuwekane sawa ,tutatue kero za wananchi kwa maslahi ya Bagamoyo,Chalinze na taifa kijumla” alisema.

Alisema asilimia ya fedha za kundi la vijana na wanawake ni lazima yatolewe kwa walengwa waweze kujiinua kimaisha .

Alieleza ,kujenga chama sio jambo la mchezo ,waungane kwa umoja wana Chalinze na Bagamoyo kufanya mabadiliko ya kimaendeleo ili kuziba upenyo kwa vyama pinzani .

Abdulsharif alibainisha kuwa ,siasa ni makundi ,ni demokrasia ,lakini uchaguzi ukiisha makundi yote yanapaswa kuwa pamoja kushikamana na kuondoa tofauti zao .

Aliwashukuru wanachama wote wa CCM ,wajumbe wa mkutano mkuu wa chama waliomchagua na ambao hawakumchagua na kusema hana kinyongo na mtu kilicho mbele ni kufanya kazi .

Katika uchaguzi uliofanyika kumchagua mwenyekiti mpya wa CCM wilayani hapo ,Abdulsharif alishinda kwa kupata kura 711 dhidi ya kura 383 za Alma’s Masukuzi huku Tariq Kifuru akipata kura 185 .

Nafasi ya Katibu Mwenezi ilikwenda kwa John Francis maarufu kama Bolizozo aliyepata kura 112 akimshinda Hassan Sharifu aliyepata kura 4

 


No comments:

Post a Comment