Mashindano ya Mazingira Kabumbu Cup 2017 Bagamoyo
yamemalizika jana Tarehe 29 Oktoba katika mchezo wa fainali uliochezwa katika
viwanja vya shule ya Sekondari Msata Halmashauri ya Chalinze kati ya Pera na
Bwilingu.
Katika mechi hiyo ya fainali timu ya Pera
imeibuka na ushindi wa goli moja dhidi ya Bwilingu na kuifanya timu ya Pera
kuchukua Kombe la Mazingira Kabumbu Cup 2017 pamoja na zawadi ya Pikipiki ya
Miguu mitatu.
Gori hilo la Pera limefungwa dakika ya 72 na mchezaji Hassani wazri ambae aliingia kipindi cha pili.
Gori hilo la Pera limefungwa dakika ya 72 na mchezaji Hassani wazri ambae aliingia kipindi cha pili.
Muanzilishi wa Kombe hilo Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo Majid Mwanga, alisema lengo la mashindano hayo ni kuifanya jamii iwe
na hamasa katika swala la kufanya usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa
jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika agizo lake la kutaka
usafi wa mazingira ufanyike nchi nzima.
Fainali ya kwanza ilifanyika katika Halmashauri
ya Bagamoyo ambapo timu ya Nianjema ilitoka na ushindi ambapo nao walichukua kombe na zawadi ya
pikipiki ya miguu mitatu.
Katika mchezo huo wa fainali mgeni rasmi alikuwa
ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ambapo alisema Wilaya ya Bagamoyo
imekuwa mfano wa kuigwa na kwamba viongozi katika maeneo mengine wanapaswa
kuiga mfano huo.
Karia aliwataka viongozi wa TFF wa mikoa na
wilaya kutoa ushirikiano pindi yanapoandaliwa mashindano kama hayo ili kuibua
vipaji vya vijana kutoka timu za chini.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema Mashindano hayo yatakuwa endelevu ili kukuza vipaji vya vijana katika taaluma ya mpira.
Kikwete alisema baada ya mashindano hayo kuisha kwa kupatikana mshindi kutoka Halmashauri ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze itaandaliwa mechi kati ya mshindi wa Bagamoyo na Chalinze ili kumpata mshindi mmoja.
Aidha, aliongeza kuwa yatafuata mashindano ya mbunge pamoja na mashindano ya chini ya miaka 20.
Kwa upande wa Bwilingu
Mbelike Ndeule, Omary Shamte, Macelo Kipresha, Ramadhani Ngandu, Mohammed Wazir, Nyange Kaburu, Samson Robson, Athuman Jungu, Azishi Saimon, Kambo Zinyori na Justine Iddi.
Kikos cha Pera
Shekhe natori, Chama iddi, Gaudensi Maarifa, Nadi Kibungo, Ramadhani Yusuph Captain, Shaibu Jongo, Abdul Muharami, Rajab Jongo, Awadhi Mohammed, Juma Mfu na Mogera Nahau.
Shekhe natori, Chama iddi, Gaudensi Maarifa, Nadi Kibungo, Ramadhani Yusuph Captain, Shaibu Jongo, Abdul Muharami, Rajab Jongo, Awadhi Mohammed, Juma Mfu na Mogera Nahau.
Kwa upande wa Bwilingu
Mbelike Ndeule, Omary Shamte, Macelo Kipresha, Ramadhani Ngandu, Mohammed Wazir, Nyange Kaburu, Samson Robson, Athuman Jungu, Azishi Saimon, Kambo Zinyori na Justine Iddi.
Mashabiki wa timu ya Pera wakifurahia ushindi.
Mchezaji wa timu ya Pera akionyesha kombe mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bwilingu.
Katikati ni Mgeni Rasmi katika mechi hiyo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Kari, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, na kushoto ni Mbunge wa jimbo la Chalnze Ridhiwani Kikwete.
No comments:
Post a Comment