Wizara zilizogawanywa ni Wizara ya nishati na
madini ambayo ilikuwa wizara moja na sasa zitakuwa wizara mbili ambazo ni Wizara
ya Nishati inayojitegemea ambayo itakuwa na naibu waziri na naibu wazriri na
wizara ya Madini ambayo pia itakuwa na waziri na naibu waziri.
Wizara nyingine iliyogawanywa ni Wizara ya
Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ambazo sasa zitakuwa wizara mbili, wizara ya kilimo
itakayojitegemea ambayo itakuwa na waziri na naibu waziri na wizara ya Mifugo
na uvuvi ambayo pia itakuwa na waziri na naibu waziri wake.
Aidha, mabadiliko mengine yamefanyika kwenye
wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ambayo sasa itakuwa na naibu waziri
wakati hapo awali ilikuwa haina naibu waziri huku wizara ya TAMISEMI itakuwa na
manaibu waziri wawili badala ya yule mmoja wa awali.
Katika mabadiliko hayo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano imeongezewa naibu waziri ambapo sasa itakuwa na manaibu waziri
wawili ambao mmoja atashughulikia mawasiliano na uchukuzi na mwingine
atashughulikia ujenzi.
Kutokana na mabadiliko hayo wizara zimeongezeka
kutoka 19 hadi 21 na manaibu waziri wameongezeka kutoka 16 na hadi 21, na
kufanya idadi ya nafasi za mawaziri zilizoongezwa ni mbili na nafasi za manaibu
waziri zilizoongezeka ni tano.
Rais Dkt. John magufuli amewataja mawaziri
walioingia kwenye Baraza jipya la mawaziri kuwa ni:-
1.Waziri
wa Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa uma na tawala bora, ni George Huruma
Mkuchika
2.Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, ni Selemani Saidi Jafo.
manaibu waziri ni Josephat Sikamba Kandege na
George Kakunda.
3.Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na
Mazingira, ni Januari yusufu Makamba naibu waziri ni Kangi Lugola.
4.Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu, ni Jenista Johakim Muhagama, Naibu Waziri kazi,
vijana na ajira ni Antoni Piter Mavunde.naibu waziri walemavu ni Stela Alex Ikupa.
5.Waziri wa kiilimo ni DKT. Injinia Charles Chizeba, Naibu waziri ni Dkt. Mere Machachu Mwanjelwa.
6. Waziri wa Mifugo na Uvuvi ni Luhaga Mpina, Naibu waziri ni Abdallah
Hamisi Ulega.
7. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ni
Prof. Makame Mnyaa Mbalawa, Naibu Waziri ni 7.injinia Etashanta Justus Nditie
na Eliasi John Kwandikwa.
8. Waziri wa Fedha na mipango ni Dkt. Philipo
Mpango, naibu waziri ni Dkt. Ashantu Kijaju.
9. Waziri wa
Nishati ni Dkt. Medadi Matogolo Kalemani, Naibu waziri ni Subira Hamisi
Mgalu.
10. Waziri wa Madini ni Angela Kairuki naibu
waziri ni Haruni S. Nyongo.
11.Waziri wa Katiba na Sheria ni Paramagamba
Kabudi.
12. Waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika
mashariki kikanda na kimataifa Dkt. Agustino Mahiga, naibu waziri Dkt. Suzani Kolimba.
13. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ni
Dkt. Husein Mwinyi
14. Waziri wa mambo ya ndani ni Mwigulu Lameki
Nchemba naibu Waziri Hamadi Yusufu Masauni.
15. Waziri wa Maliasili na utalii ni Dkt. Hamisi
Andrea Kigwangwala naibu waziri ni Ngailonga Josephati Hasunga.
16. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi ni Wiliamu Lukuvi naibu waziri Engelina Sylvester Mabula .
17. Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji ni
Charles Paul Mwijage naibu waziri injinia Stela Manyanya.
18. Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi ni Joyce
Ndalichako Naibu waziri ni Wiliamu Ole nasha.
19. Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto ni Ummy Mwalimu naibu wake ni 19Faustin Ndungulile.
20. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ni Dkt. Harson George Mwakyembe, naibu wake ni 20Juliana Daniel Shonza.
21. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, I sack Aloece
Kamwelwe naibu wake ni Juma Hamidu Awesu.
Aidha, Rais Dkt. Magufuli amefanya mabadiliko kwa
katibu wa Bunge na kumteua Dkt. Stephen Kagaigai.
Rais Dkt. John Magufuli alisema wateule wote
waliotajwa wataapishwa jumatatu Tarehe 09 Oktoba 2017.saa tatu Asubuhi.
No comments:
Post a Comment