Kulia
ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, akiweka jiwe la msingi nyumba mbili za askari magereza katika gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo, kushoto ni Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo.
Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP. Muyengi Bulilo. (aliyeshika karatasi mkononi) akimunesha nyumba za askari zinazojengwa katika Gereza hilo.
........................
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt.
Juma Aliy Malewa, ameweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba mbili za Askari
magereza na kuzindua jengo la wageni katika Gereza la Kigongoni wilayani
Bagamoyo.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi
na kuzndua jengo la wageni,CGP. Dkt. Juma Malewa alisema magereza zote hapa
nchini zinakabiliwa na changamoto za kukosa nyumba za kuishi Askari na kwamba
mkakati uliopo ni kujenga nyumba hizo kwa kutumia nguvu kazi iliyopo ndani ya
magereza.
Aidha, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha
inaondoa tatizo la nyumba za Askari magereza kwenye magereza yote hapa nchini
na kuongeza kuwa katika kuhakikisha lengo hilo linatimia, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania hivi karibu alitoa pesa kiasi cha shilingi Bilioni 10
ambazo zitatumika kujenga 380 za askari magereza katika gereza la Ukonga jijini
Dar es Salaam.
Awali akitoa taarifa mbele ya Kamishna Jenerali
wa Magereza, Mrakibu wa Magereza SP. Muyengi Bulilo alisema nyumba hizo zinajengwa
kwa kutumia nguvukazi waliyonayo gerezani na hivyo kuokoa kiasi cha pesa
ukilinganisha na ujenzi wa kutumia nguvu kazi za nje ya gereza.
Alisema nyumba hizo mbili kila moja itakuwa na
familia tatu hivyo nyumba hizo zitakapokamilika zitachukua familia sita za
askari magereza na hivyo kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba za askari katika
gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt.
Juma Aliy Malewa,(kushoto) akizindua jengo la wageni katika gereza la Kigongoni Bagamoyo
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, katikati akifurahi pamoja na maafisa wa jeshi la magereza mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la wageni pamoja duka katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo, kulia ni mkuu wa Gereza hilo la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza SP. Muyengi Bulilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP, Dkt. Juma Aliy Malewa, akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo, pamoja na maafisa wa jeshi la magereza katika Gereza la Kigongoni Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment