Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tate
Wilimu Ole nasha amewatoa hofu wakazi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayosi
wilayani Bagamoyo ambao wamepakana na Ranchi ya Ruvu na kuwataka waendelee na
shughuli zao za kilimo kama kawaida wakati wakisubiri maamuzi ya kupitia upya
mipaka ya Ranchi ya Ruvu.
Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo alipotembelea
katika kijiji cha Mkenge na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu
Ranchi ya Ruvu kuingilia mashamba ya asili ya wanakijiji hao jambo ambalo
linasababisha usumbufu na kukosa sehemu ya kulima.
Aidha, naibu waziri huyo wa kilimo, Mifugo na
uvuvi, aliwataka wenyeji wa kijiji hicho kuacha kuwakaribisha wageni kuja
kuweka makazi katika maeneo hayo kwani kwa kufanya hivyo kutavuruga mpango wa
serikali wakuandaa mipango ya kurekebisha mipaka.
Alisema kwa sasa wananchi wa kijiji hicho
wanaweza kuendelea na shughuli zao za kilimo na kwamba maamuzi ya serikali
yatakapotolewa hayawaathiri wananchi hao na kuwataka kuwa na subira na kufanya
shughuli zao kilimo kwa amani na utulivu.
Wakati huo huo, Nibu Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi aliwataka wafugaji kuheshimu mashamba ya wakulima na kuacha kupeleka mifugo kwenye mashamba.
Alisema vijiji vimeandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya wafugaji na wakuli hivyo kila mmoja afanye shughuli zake kwenye maeneo ambayo ameruhusiwa kisheria bila ya kuingiliana.
Naibu waziri, Ole nasha, aliwataka makabila mawili jamii ya wafugaji, wamasai na wabarberi kuacha tofauti zao na badala yake wakae pamoja kwa maelewano.
Alisema kitendo cha kutokuelewana baina ya wamasai na wabar beri kunapelekea kundi moja kuhama sehemu waliypangiwa na hatimae kusababisha wavamizi wa maeneo ambayo sio rasmi kwa ufugaji.
Nae Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alimshukuru naibu Waziri huyo kwa kufika katika kijiji cha Mkenge ili kusikiliza kero za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimsumbua kuhusu mgogoro wa mipaka kati yao na Ranchi ya Ruvu.
Awali wananchi, wakazi wa kijiji cha Mkenge walimueleza Naibu waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi kuwa wanapata usumbufu kwenye mashamba yao baada ya Ranchi Ruvu kuwataka kuondoka kwenye mashamba hayo ili kupisha hifadhi ya Ranchi jambo ambalo linapelekea kushindwa kuendelea na shughuli zao za kilimo.
Diwani wa Kata hiyo ya Fukayosi, ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy Issah, alimuomba Naibu waziri huyo kuangalia uwezekano wa kuwaachia wananchi wakazi wa kijiji cha Mkenge maeneo yao ya kulima ambayo wamekuwa wakilima hapo kwa miaka mingi iliyopita.
wananchi wakazi wa kijiji cha Mkenge wakimsikiliza Naibu waziri wa kilimo, Mifugo na uvuvi, Wiliamu Ole nasha alipotembelea kijini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, akimkaribisha Naibu waziri wa kilimo, Mifugo na uvuvi kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Mkenge.
No comments:
Post a Comment