WASIFU
WA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SALUM ALLY MKANGAMBE
KUZALIWA KWAKE.
KUZALIWA KWAKE.
AMEZALIWA MWAKA 1969 KATIKA KATA YA MWEMBESONGO AKIWA MTOTO WA TATU WA MZEE SALUM MKNGAMBE NA MTOTO PEKEE KWA UPANDE WA MAMA YAKE.
ELIMU YAKE;
SHEIKH ABDALLAH SALUM ALLI MKANGAMBE ALIANZA ELIMU YAKE YA MSINGI KATIKA SHULE YA MTAWALA ILIYOPO MANISPAA YA MOROGORO KUANZIA MWAKA 1978-1984.
AIDHA MWAKA HUOHUO SHEIKH MKANGAMBE AKIWA KIJANA WA MIAKA TISA, ALIANZISHWA ELIMU YA AWALI YA DINI YA KIISLAMU KATIKA ENEO LA MAGUBIKE WILKAYANI KILOSA.
MNAMO MWAKA 1981 ALIANZA RASMI MASOMO YA QUR’AN KWENYE AMANI MADRSA ILIYOKUWA CHINI YA MAREHEMU SHEIKH SAID MUSSA KARIYAT.
SEPTEMBA 27/1985 ALIKWENDA DAR ES SALAAM NA KUJIUNGA NA CHUO CHA MARKAZ MNAMO OKTOBA 1985-1990.
MWAKA 1990 BAADA YA KUFAULU MITIHANI YAKE YA MWISHO, ALIFANIKIWA KUWA MIONGONI MWA WATANZANIA WANNE WALIOPATA NAFASI YA KWENDA NCHINI MISRI KUENDELEA NA MASOMO YA JUU KATIKA CHUO KIKUU CHA AZIHAR-SHARIIF.
OKTOBA 1990-1993 MASOMO YA SEKONDARI (THANAWIY) ALEXANDRIYA, MISRI NA KUFAULU VIZURI.
OKTOBA 1993-1997 ELIMU YA CHUO KIKUU KITIVO CHA SHERIA, CHUO CHA AZHAR-SHARIF KAIRO, MISRI.
KAZI ZAKE;
MWAKA 1984-1985 MWALIMU MADRASA YA AMANI NA UHURU
MWAKA 1997-1998 MAREHEMU SHEIKH MKANGAMBE BAADA YA KUREJEA MASOMONI, ALIANZA KUFUNDISHA CHUO CHA AMANI KILICHOANZISHWA NA SHEIKH WAZIRI MADUGA MWAKA 1996.
MWAKA 1998 MWALIMU WA DINI SHULE YA SEKONDARI JABAL-HIRAH, MOROGORO.
JANUARI 1999 ALIAJIRIWA NA AFRICAN MUSLIM AGENCY NA KUWA MWALIMU WA NIDHAMU (DISCPLINE MASTER) KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU YA WASICHANA YA ATTAWN, MOROGORO.
MWAKA 2009-2010 ALIPANDISHWA DARAJA NA KUWA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA KIISLAMU YA ATTAUUN.
MWAKA 2011-2012 ALIKUWA MKUU WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA AL SAFFAH YA MJINI MTWARA ILIYOKUWA CHINI YA AFRICAN MUSLIM AGENCY .
MWAKA 2012 ALIREJEA MOROGORO NA KUENDELEA NA KAZI YAKE YA UWALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA ATTAWN KAMA MWALIMU WA NIDHAMU KABLA MWAKA 2013 KUTAKIWA TENA MTWARA AL SAFFAH SEKONDARI KUWA MKUU WA SHULE.
DESEMBA 2013 SHEIKH MKANGAMBE ALIACHA KAZI NA KURUDI MOROGORO NA KUWA MWALIMU MKUU MSAIDIZI KATIKA SHULE YA MSINGI YA KIISLAMU YA AL-HAQABA ILIYOPO MAFISA.
MPAKA MAREHEMU ANAFIKWA NA UMAUTI ALIKUWA MKUU WA IDARA YA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA JABAL-HIRRAH.
UZOEFU KATIKA UONGOZI;
MWAKA 2005-2010 SHEIKH ABDALLAH SALUM MKANGAMBE ALICHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MASHEIKH MKOA WA MOROGORO.
MWAKA 2010-2015 SHEIKH ALICHAGULIWA KUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA BAKWATA MKOA WA MOROGORO
NA KUANZIA MACHI 27, 2016-OKTOBA 17, 2017 ALIKUWA AKIHUDUMU KATIKA NAFASI YA SHEIKH WA MKOA WA MOROGORO, MJUMBE WA KAMATI YA AMANI NA MJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA SHULE YA SEKONDARI YA JABAL-HIRRAH.
TANGU ACHAGULIWE KUSHIKA NAFASI YA SHEIKH WA MKOA WA MOROGORO MWEZI MACHI, 2016, MAREHEMU SHEIKH MKANGAMBE ALIKUWA MHAMASISHAJI MKUBWA WA WAISLAMU KUMILIKI ARDHI KWA AJILI YA MAENDELEO YAO.
LAKINI PIA NI KIONGOZI PEKEE AMBAE ALIWEZA KUTEMBELEA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MOROGORO NA BAADHI YA VIJIJI VYAKE KATIKA KIPINDI KIFUPI CHA UONGOZI WAKE.
AIDHA
KUTOKA MWAKA 2005 MPAKA MUDA MFUPI KABLA YA UMAUTI WAKE, MAREHEMU SHEIKH
MKANGAMBE ALIKUWA KIONGOZI MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA KIISLAMU MKOANI MOROGORO.
MAREHEMU PIA KWA MIAKA MINGI ALIKUWA AMEJITOLEA KUFUNDISHA ELIMU YA DINI KATIKA MADRASA MBALIMBALI ZA MJINI MOROGORO PAMOJA NA KUTUMIA VITUO VYA HABARI KAMA VILE RADIO MUM NA IMAAN MEDIA KUFIKISHA UJUMBE KWA JAMII.
TUNAMUOMBA
MWENYEZIMUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SALUM ALLI MKANGAMBE
MAHALA PEMA PEPON. AAMIN!
SISI SOTE NI WA MWENYEZIMUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.
SISI SOTE NI WA MWENYEZIMUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.
IMEANDALIWA
NA RASHID MTAGALUKA
...........................................................
RATIBA
YA MAZISHI YA MAREHEMU MKANGAMBE.
TAARIFA
ILIYOTOLEWA JANA NA MSEMAJI WA MUFTI WA
TANZANIA
IMESEMA
MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SALIM MKANGAMBE
ATAZIKWA LEO ALHAMISI TAREHE 19 OKTOBA 2017.SAA SABA MCHANA NYUMBANI KWA MAREHEMU
MOROGORO
No comments:
Post a Comment