Waziri
wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamad Al–Rumhi
akitazama jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo wakati wa
ziara yake wilayani Bagamoyo leo.
Waziri huyo ametembelea maeneo ya uwekezaji
ya Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA), maeneo ya Kihistoria
la Kaole na eneo itakapojengwa Bandari, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Mhandisi Stellah Manyanya, nyuma ya Naibu waziri Viwanda ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga.
Waziri
wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamad Al–Rumh
akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi
(EPZA) Kapteni George Simbakalia alipokuwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya
uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo.
Naibu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya akipokea
zawadi toka kwa Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin
Hamed Al–Rumhi wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani
Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Hemed.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy leo Tarehe 19 oktoba alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari Bagamoyo.
Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed
Hamad Al Rumhy (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa chuo cha Wakala wa Mafunzo na
Elimu ya Uvuvi Mbegani (FETA) Yahya Mgawe, alipotembelea Mbegani Bagamoyo leo
katika eneo ambalo litajengwa Bandari ya Bagamoyo, wanaoshuhudia kutoka kushoto
ni wa Tanzania nchini Oman Abdallaah kilima na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa
wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Mafuta na
Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamad Al–Rumhy, Balozi wa Oman
nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al Mahruqi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj
Majjid Hemed wakimsikiliza mhifadhi ya makumbusho ya Kaole Bagamoyo walipotembelea
eneo hilo leo Tarehe 19 Oktoba 2017.
No comments:
Post a Comment