Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano cha mbweni,
Beatrce Njanda pamoja na katibu wa kikundi hicho Florence lema, wakigawa msaada
wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa wazee wanaoishi
katika kambi ya Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam, vitu hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Sabuni za
kufulia na kuogea, Dawa za meno na miswaki, mafuta ya kupaka, nguo, juisi Nk.
Ojuku Mgedz ni Msimamizi wa kituo katika kambi hiyo ya
wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Slaam, akiwakaribisha kinamama ambao ni wananchama wa kikundi
cha mshikamano cha Mbweni walipofika katika kambi hiyo kutoa misaada ya viyu
mbalimbali leo Tarehe 14 Oktoba 2017.
Mmoja wa wazee hao akipokea msaada uliotolewa na
kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni, katikati ni Mwenyekiti wa
kikundi hicho, Beatrce Njanda pamoja na katibu wa kikundi hicho Florence lema, walipotembelea kambi ya wazee iliyopo Nunge Kigamboni jijini Dar es Aalaam.
Mmoja wa wazee hao waliopata msaada wa vitu mbalimbali kwa kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni.
Kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni wakiwa katika harakati za kugawa msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee wanaoishi katika kambi ya wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Kikundi hicho kinaongozwa na Mwenyekiti Beatrce Njanda, Makamo Mwenyekiti Grace Magembe, Mweka hazina Judithi manongi, Katibu Florence lema, Katibu msaidizi Veronica Mchele.
No comments:
Post a Comment